Ni yule yule mdau na mpenzi wa kupashana habari kwa kupitia blog tofauti na wadau wenzangu. 

Mie niko Gothenborg Sweden, na tunafuatilia mambo mengi yanayo likumba taifa letu, lakini kunabaadhi ya mambo hatukubaliani nayo na watanzania wanayafumbia macho. Mimi kila mwaka lazima nije nyumbani kuangalia ni fanye nini ili niweze kuanzisha ajira kwa baadhi ya ndugu zetu wenye vipato vya chini namaanisha kufungua miradi yangu na kuajiri watakao iendeleza kwa manufaa yetu kati yangu na wao pia na taifa kwa mfumo wa kulipa kodi. 

Lakini kuna jambo linalotupa wasiwasi katika system au niseme MFUMO uliopo katika nchi yetu wa kwamba Mtz atakae chukuwa uraiya wa nje basi atakuwa ameukana utanzania, sasa tunajiuliza (KUNATOFAUTI GANI KATI YA TZ NA NCHI ZINGINE ZA KIAFRIKA ZILIZO RUHUSU URAIYA MARA 2 AU 3?) Jee Kaka Michuzi hata kama ni wewe unaweza kuingiza mtaji shimoni na huku unaliona shimo??? Kuchukua uraiya wa nchi husika ni kutaka kurahisisha maisha ya hapo mtu alipo ili aweze kujikim na kupata zile haki za msingi pamoja na kuanzisha kitu kidogo nyumbani.

Ukiangalia wenzetu Nigeria, Senegal, Burundi, Rwanda watu wao waishio nje wanakubaliwa kuchukuwa uraiya wa huko waliko na bado wanashikilia uraiya wao. Maana hata kama wewe ni Muhindi ukachukuwa uraiya wa Tanzania ni karatasi tuu lakini wewe hujabadilika kuwa Mtanzania damu. Ninayo shughuli yangu hapa lakini nafikiria ingekuwa kwetu ningefanya makubwa kuliko haya ninayofanya hapa Europe, maana kwetu bado tunahitaji huduma kibao ambazo kwa sisi tuishio n'nje tunaziona na zinalipa, na wenzetu waishio Bongo wanaweza kuiga na kujiendeleza wakafanikiwa pia. 

Swali ni kwamba hali hii itaendelea hadi lini na kama serikali imeshaa ruhusu tunaomba swala hili liwekwe wazi bayana kila mtun asikie na ajuwe, tumepekuwa hadi kwenye mtandao wa Ubalozi wa Tanzania hapa Sweden hakuna sehemu inayo onyesha kuwa Mtanzania anaruhusiwa kumiliki passport 2, na hii imetokana na ubishi wa baadhi wakisema eti MTZ kwa sasa anaruhusiwa kumiliki pasi 2, na htakiwi kulipa visa unapo ingia Tanzania kitu ambacho tumekuta sio kweli ni maneno tuu ya Wabongo. 
 
INSHA-ALHAH. 
 
Ahsante
Wako ADAMS CHUMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Sio muhimu sasa hivi. Tutatue kwanza yanayoendelea nchini. Mpaka wa Malawi, kuuwawa kwa wanahabari, kukataa kuhesabiwa Waislamu, umasikini, umasikini na umasikini wa Watanzania walio wengi na ambao hawatafaidika direct na huo uraia wa nchi mbili.

    ReplyDelete
  2. Ndugu Mtoa hoja Mimi nitakujibu Suala Lako kwa kifupi mataifa kadhaa ya afrika Ambayo umeyataja baadhi na kuisahau Ghana Ambao nao wameruhusu Uraia wa nchi Zaidi ya moja,wenzetu hawakuwa na viongozi au mfumo aw kikomunisti kwa Muda mrefu kuna walikuwa nao mfumo huo kwa Muda mfupi baadae viongozi hao waliuwawa au waliondolewa kwa Kura na kuna nchi Ambazo hawaku adopt siasa za mashariki kabisa sasa generation za viongozi wao aw sasa na hata wale wa zamani wana mitizamo inayokwenda na wakati tulionao duniani kwa sasa sasa tune bongo CCM na viongozi wake karibu wote ni Matunda ya mwalimu Nyerere na swali jepesi Jiulize Kama mwalimu angekuwa hai angekubali jawabu Hapana sasa unategemea nini kutoka kwa wanawe Hawa Mimi nasubiri wamalizike wote labda tukianza kupata vizazi vipya Ambao hawajui chochote kuhusu ujamaa,Nyerere na CCM hivi sasa wanapandikiza watoto wao ndani ya Chama hicho kwa maana hiyo hicho kitanzi kipya ndani ya CCM hawana jipya Mimi nakushauri subiri mabadiliko ya siasa kwa Tanzania yatachukua Muda si mrefu kuanzia sasa hapo Ndio huo mfumo utawezekana.

    ReplyDelete
  3. Mimi pia ni mbongo niliye hapa europe na nina passport ya huku kwa maslahi zaidi ila bado naipenda bongo na ni nyumbani ila cha kushangaza hili suala la uraia wa nchi mbili ambapo cha kushangaza kuwa serikali inapinga kuwa na passpoti mbili ni maajabu makubwa sana.Ikizingatiwa mimi ambaye ni mbongo ninayeishi huku ninasaidia watu kibao ,kuwasomesha ndugu kibao na marafiki na hii ni kwa manufaa ya taifa pia.Kama ningekuwa na passpoti mbili ningeweza kufungua biashara kubwa zaidi na kuwekeza zaidi nyumbani ili kutoa ajira kwa wabongo na pia kulipa kodi kwa serikali,ila cha ajabu sijui ni kwa nini serikali yetu inapinga jambo hili?Ikizingatiwa ni kwa manufaa zaidi ya taifa na sio laa.Hivyo nawaomba wananchi ,viongozi ktk kipindi hiki cha kupitia maoni ya katiba mpya hili jamba liwekwe huko ktk katiba mpya kwa manufaa ya taifa ,kwani ukizingatia kipato kikubwa sana cha taifa kinatokana na wabongo waishio nje ,bro. michuzi ukitaka kujua hili waulize western union kila mwezi ni wabongo wangapi wanaotuma fedha huko nyumbani etc.Hili suala siyo la kufumbia macho ni la muhimu sana.Aksante mdau uliotoa mada hii ,aksante bro michuzi kwa kuniwezesha kutoa maoni.Big up mdau ,big Joe ughaibuni

    ReplyDelete
  4. Unajua sababu kubwa ya kutofanya hivyo ni hakuna sababu yakufanya hivyo. Na wewe uliye sweden hao ndugu zako ni wa sweden au? Au unataka kuanzisha biashara zako mwenyewe.. This is non issue na isitupotezee muda. kama wewe umepewa uraia wa makaratasi na hiyo inchi haijakungang'anya passport ya nchi yako Tatizo liko wapi? Mimi nawajua watu kibao ambao ni raia wa nchi nyingine lakini wanaendeleza mambo yao kama kawaida bongo na hiyo serikali ya CCM wala haiwafanyi kitu wala nini na wengine wana vyeo vikubwa tu ..Kama unataka kuanzisha biashara nenda kaanzishe kwa jina lako au ndugu zako hakuna noma wala nini.. Mbona kuna raia wa nje wako bongo wanafanya biashara vizuri tu kwa nini wewe ushindwe. Mimi sioni sababu ya kuzuia uraia wa nchi mbili na pia sioni sababu ya kukataza kwa hiyo hii ni non issue kuna matatizo mengi tu ya kushughulikia kabla ya hili.

    ReplyDelete
  5. yeyote anayeishi Bongo na hajawahi kusafiri si rahisi kuelewa nini maana ya watu wa ughaibuni kulalamikia uraia pacha.Nashangaa hadi sasa Zebedayo msema kweli hajacomment topic hii maana yeye kila jambo zuri la ughaibuni ATALIPINGA!!!Anyway ni kweli kuna matatizo mengine muhimu Bongo lakini na hili nalo kwa sisi wa ughaibuni linatusumbua sana na hasa tukiangalia kuwa hakuna sababu yoyote ya kimsingi ya kulizuwia hadi sasa.

    ReplyDelete
  6. Mie naona kuna vibaka wenye malengo yao na kutoa mada mbali mbali kupima watu wanasema kuhusu issue mbali mbali. Sasa kama jamaa wa hapo juu Anonymous Tue Sep 18, 02:43:00 AM 2012 anaona siyo issue labda kwa vile yeye ndiye ndugu zake wako kwenye ngazi nyeti za serikali na wanaogopa jamaa toka nje'wakirudi itakuwa imekula kwao. Nimechoka kuona vyama vya siasa vikitumia watu wa ughaibuni kama kete za kamali. Wanapotaka michango ya uchaguzi ndio wanakuja kujifanya watashughulikia hiyo issue ya uraia pacha. Mie nitakumbuka chama kitachofanikisha hii issue, na nitakiadhibu chama ambacho kilikwenda vingine. Na sasa CCM ilitoa ahadi miaka 5 iliyopita lakini inaonekana dhaifu.

    ReplyDelete
  7. Uraia wa Nchi zaidi ya Moja,

    Hili suala ni la Tija zaidi kwa nchi kwa kuwa kila Taifa linahitaji ukuaji ktk sekta za:

    -Uchumi/Economy, Madiaspora wamethibitishwa kujenga uchumi wa nchi zao asilia kwa kutuma Fedha kwao na kuwekeza kiuchumi na kuchangia maendeleo.

    -Umaihsaji wa kuleta Teknolojia nchini/Technology Transfer,
    Madiaspora wanahamishi Teknolojia nyumbani kutoka Ughaibuni kama wewe Mdau Chuma unavyotaka kufanya.

    -Ulinganishi wa Upungufu wa wafanyakazi /Labor-Fiscal Deficit and so on.
    Madiaspora wanasaidia kutosheleza upungufu wa mahitaji ya Taaluma ktk Uchumi wa nchi kwa zile Taaluma ambazo nchi ina upungufu wake.(Mfano Mtanzania Dakitari wa nje akifungua shughuli zake nchini atakuwa ameiwezesha nchi kimtaji na kitaaluma huku akichangia maendeleo nchini Tanzania)

    Zaidi ya hapo pana tahadhari za Kiusalama kwa kuwa maadui na wahalifu wanaweza kutumia mwanya huo kutimiza azma zao.

    Pia ili kuleta uhakika zaidi ktk nchi nyingi watu wenye Uraia wa nchi zaidi ya moja ama Raia wa kuandikishwa hawashiriki mambo yote nchini, mfano wanaruhusiwa kupiga kura, wanaweza kufanya kazi Serikalini kwa ngazi fulani lakini hawaruhusiwi ngazi nyeti na kugombea ngazi fulani za Uongozi.

    ReplyDelete
  8. Nchi zote ya Afrika Masharika zimeshakubali uraia wa nchi mbili.
    Kenya, Uganda na Rwanda na zote
    zinasifu mafanikio walopata baada
    ya kuruhusu.

    ReplyDelete
  9. Waughaibuni mnasemaje ? Tuishinikize serikali kupitisha swala hili la Uraia wa nchi mbili katika katiba yake mpya.
    Kama Serikali itashindwa, basi iruhusu wa huku tuwe huku na wa kule kule.
    Na tukiwa na Chama imara basi itabidi tulazimishe umoja wa mataifa uruhusu kuleta ndugu zetu huku tuishi nao huku na kwa njia hiyo si vibaya tukikosa wote.
    Yeyote anaye pinga hoja hii akumbuke mtoamaoni anahaki ya kuishi kwenye mchi yake kihalali.
    Pia mtu yeyote anaruhusiwa kuwa mkimbizi wa kiuchumi katika nchi yoyote na akakubalika.
    Michuzi wazuuup we uchangii hoja hii?Usitutupe machizi wako wa ughaibuni.

    ReplyDelete
  10. HATUTAKI MAPOPO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Kuwapa Pasipoti mbili na kuwa na Uraia Pacha sio jambo gumu,

    ISIPOKUWA CHONDE CHONDE MARA NYINGI NDUGU ZETU MLIOPATA URAIA WA NJE MNAHESHIMU SANA PASIPOTI ZENU NA URAIA WENU SAMBAMBA NA KUTII SANA SHERIA ZA HUKO MLIKO KULIKO HUKU.

    HIVYO TUSIJE WAPA PASIPOTI YETU NZURI SANA YA 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA' HALAFU MKAITUMIA VIBAYA PASI HIYO KWA KUSAFIRISHIA MADAWA YA KULEVYA NA SHUGHULI HARAMU!

    SAMAHANI NAWAKILISHA!

    ReplyDelete
  12. Wandugu zetu Majuu,

    Sio balaa wala nini sisi kuwapatia Pasipoti ya nyumbani Tanzania.

    Isipokuwa wengi wenu tokea mfike huko mmebadilika sana mpo kimaslahi zaidi kuliko Uzalendo, sio tuwapeni Pasi za Tanzania halafu mchukue Pasi zenu za Sweden na Ujerumani muweke sandukuni halafu mchukue Kitabu cha Tanzania kwenda kubebea madawa ya unga huko shamba!

    Lohhh, kwa nini tusiwachunguze kwanza kabla ya kuwapatia Pasi?

    ReplyDelete
  13. Ehhh tumeshituka!

    Wewe uweke kibindoni Pasi yako ya Norway halafu uchukue Pasi ya Jakaya Kikwete ukabebee Madawa ya Ulevi Brazil?

    ReplyDelete
  14. Uraia Pacha:

    Kama Penzi haligawanyiki na vivyo hivyo na Uzalendo haugawanyiki!

    Huwezi ukawa unatumikia wapenzi wawili kwa wakati mmoja na wote ukawatendea ama kuwapa penzi sawa lazima utaelemea sehemu moja.

    Ndugu zetu wa Majuu mnaonesha kila dalili kuwa mtaegemea zaidi huko ingawa mtakapo pewa na huku, na ndio kama hapo juu Wadau wengine wamesema mnaweza kuitumia Pasi ya TZ vibaya huku mkiiheshimu na kuikweza Pasi ya Majuu.

    Simtaji jina, jamaa yangu mmoja wa Canada huwa akija Bongo, Pasi yake ya huko anakaribia kuiabudu akifika tu akitua Bongo kitu cha kwanza anaikabidhi kwa Bi. Mkubwa amtunzie !!!

    Sasa mtu wa namna hii tunaweza mchukulia vipi ?,,,ni kweli anaweza kuipa uzito Pasi ya pili (ya Tanzania)akipewa kama anavyoifanya karibia kuiabudu ya Canada ?

    ReplyDelete
  15. Anonymous wa Wed Sep 19, 01:58:00 PM 2012, Wed Sep 19, 01:56:00 PM 2012,na Wed Sep 19, 11:27:00 AM 2012

    Kwa hiyo mamilioni ya watanzania walioko nje' kazi yao ni kubeba madawa? Hiyo pasipoti ya TZ ndiyo inaruhusu kubeba madawa kirahisi. Jamani wakati mwingine mnatia haibu na hoja zenu. Mnajitia aibu wenyewe kwa kusema WaTZ mnabeba madawa, hivi hamuoni mnajisema??!! kama hauna point siyo lazima uchangie. Uhuru wa kusema siyo lazima kuropoka. Kwa mfano huwezi kuropoka "moto" kwenye nyumba ya sinema iliyojaa watu ambapo hamna "moto". utahatarisha maisha ya watu bure.

    ReplyDelete

  16. Mbona hao vigogo wote wananduguzao huku ,inamaana ndiyo wanawauzia madawa ya kulevya?
    Au tuorodheshe majina ya ndugu wa vigogo walio ughaibuni na wanaishi vipi?
    Nyinyi jibuni swali kama wa huku wawe wa huku na wa huko huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...