Ndugu Watanzania na wapenzi wa ngumi za kulipwa. Ili kuweka sahihi taarifa nyingi nzuri kuhusu msuala ya ngumi za kulipwa na ambazo tunafurahi kuwa zimeanza kutolewa na bwana Yasin Abdallah (Ustaadh), tungependa pia kuwapa maelezo sahihi kuhusu ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Ubingwa huu umekuwa unapigiwa kelele na baadhi ya watu ambao wana malengo ya kuharibu taswira nzima ya nguni za kulipwa na kuturudisha nyuma kwenye enzi za vurugu zilizowahi kutokea hapo nyuma.
Ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ulianzishwa mwaka 1983 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Mpaka kufikia wakati huo (1983) ni nchi ya Tanzania peke yake iliyokuwa imeshaanzisha ngumi za kulipwa katika ardhi yake ambapo Kenya na Uganda zilikuwa bado hazijaanzisha ngumi za kulipwa nchini mwao japokuwa zilikuwa na mabondia kadhaa waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa katika nchi za Ulaya na Asia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...