Ndugu Watanzania na wapenzi wa ngumi za kulipwa. Ili kuweka sahihi taarifa nyingi nzuri kuhusu msuala ya ngumi za kulipwa na ambazo tunafurahi kuwa zimeanza kutolewa na bwana Yasin Abdallah (Ustaadh), tungependa pia kuwapa maelezo sahihi kuhusu ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Ubingwa huu umekuwa unapigiwa kelele na baadhi ya watu ambao wana malengo ya kuharibu taswira nzima ya nguni za kulipwa na kuturudisha nyuma kwenye enzi za vurugu zilizowahi kutokea hapo nyuma.
Ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ulianzishwa mwaka 1983 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Mpaka kufikia wakati huo (1983) ni nchi ya Tanzania peke yake iliyokuwa imeshaanzisha ngumi za kulipwa katika ardhi yake ambapo Kenya na Uganda zilikuwa bado hazijaanzisha ngumi za kulipwa nchini mwao japokuwa zilikuwa na mabondia kadhaa waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa katika nchi za Ulaya na Asia.



ILI IWEJE!!?
ReplyDelete