Kamati ya Jumuiya ya Madaktari Nchini , kwanza inapenda kutoa pole kwa Wanahabari wote nchini kwa kitendo cha kinyama ambacho Mwanaharakati na Mwandishi wa habari, Marehemu David Mwangosi alifanyiwa, hii ni ishara kuwa Jeshi la Polisi wameamua kutumia njia ya kuua raia ili kujenga hofu na woga miongoni mwa wapenda demokrasia na maendeleo nchini.

Pia tunapenda kulaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni kulifungia gezeti makini la Mwanahalisi kwa sababu ya kutoa taarifa za ukweli juu ya waliotaka kukatiza uhai wa Dr.Ulimboka Stephen, Jamii ya Madaktari na watanzania wengi bado wanaamini kuwa waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi ni miongoni mwa waliohusika na kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwake na si yule anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliyedaiwa kukamatwa na Suleimani Kova. Hivyo tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ripoti yake ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hii.

Pia, tunachukua nafasi hii kupongeza mshikamano ambao Madaktari wameendelea kuuonyesha licha ya changamoto nyingi tunazopitia, ni vema ikafaamika kuwa ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa MAT na MAT imefunguliwa kesi 2 mahakamani, Ni katika kipindi hiki ambacho zaidi ya interns 300 wanasubiri kuitwa kuhojiwa na MCT bila kujua ni lini hilo litafanyika, Ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari anapata mapumziko baada ya kutoka katika Matibabu nchini Afrika Kusini, lakini ni katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa hakuna hata hoja moja ya Madaktari imefanyiwa kazi na Serikali.

Tunapenda ieleweke kuwa suala la madai ya Madaktari si tukio, ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndio maana tumeshuhudia migomo hii katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslai ya watumishi kwa ujumla.

Kuhusu suala la interns, Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 10, Julai 2012, Baraza la Madaktari Nchini lilitoa taarifa kwa umma kuwa imesitisha leseni za muda kwa Madaktari waliochini ya mafunzo kwa vitendo, pia waliahidi kuwaita kwa nia ya kuwahoji mmoja mmoja pindi wakatapokamilisha uchunguzi wao, cha kushangaza ni kwamba miezi 2 sasa imepita bila hilo kufanyika.

Katika vikao mbalimbali ambavyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, na Kaimu Katibu Mkuu wameshiriki, wamekuwa wakisisitiza kuwa hili lipo kisheria na interns wasuburi kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa. Hivyo tunapenda kutumia nafasi hii kuitaka MCT itekeleze kwa haraka majukumu yake kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki.

Hivyo basi Kamati ya Jumuiya ya Madaktari imejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na itahakikisha inaweka wakili pale interns watakapoanza kuhojiwa kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa hiyo nafasi.

Mwisho kabisa tunapenda kutoa wito kwa interns kutumia hekima na busara katika kipindi hiki kigumu, waepuke kutumiwa na kikundi cha watu ambao wanatumika au wanajitumia kwa maslai ya kustarehesha watawala.

                           IMETOLEWA NA; KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nyie mi wataalamu tena adimu msirubuniwe daini chenu tena kwa msimamo na msitishiwe!

    Wabunge wanaruka na milioni 11 kwa mwezi wao wanazipata kwa utaalumu upi?

    ReplyDelete
  2. Milioni 11 kwa mwezi ni Mshahara wa Daktari Bingwa Uingereza ambaye ana experience ya miaka kumi hivi.

    ReplyDelete
  3. SWALA HILI NI KWA WATANZANI WOTE KUSIMAMA PAMOJA KUWASAIDIA MADAKTARI KUPATIWA VITENDEA KAZI NA TUACHE SIASA NA USHABIKI WA KIJINGAAAAAAAAA,,,,,,,,,

    ReplyDelete
  4. umma ni sisi,watanzania ni sisi ,acheni kazi hatuwataki kabisa, nendeni mkafanye siasa.

    ReplyDelete
  5. Hii taarifa ina harufu kama ya kisiasa siasa vile. Au pua zangu zishakuwa chakavu?

    ReplyDelete
  6. Wewe anny wa 01.00 then kazi za udaktari afanye nani? unafikiri ni siasa hii? hebu kwa mfano angalia ktk UKOO wenu utakuta hakuna dr. hata mmoja na hata baada ya miaka 100 ijayo bado hakuna! kuwa Dr. lazima uwe na KICHWA! lkn ktk ukoo wenu wanasiasa UCHWARA utakuta wapo kama 50 hivi!
    Tatizo lako una UTAPIA MLO WA KUFUKIRI

    ReplyDelete
  7. Inanisikitisha sana mahala tulipofikia kuhusu hili swala la utoaji wa tiba na masilahi ya Madaktari Tanzania.
    Kwa wenzetu waliostarabika siku nyingi kidogo, na wanaowajali watu wao na afya zao, wasingefikia hapa tulipo leo.
    Afya ni haki ya kila mwananchi kwa jamii zinazoelewa umuhimu wa afya na uchumi.
    Afya sio swala la kujadiliwa na watu wakiwa bar, sokoni au kwenye vyombo vya habari, mitandao au kupelekwa bungeni.
    Kuzungumzia swala la afya linahitaji Wataalamu wa afya, muda wa kutosha wa kujadili kwa makini vipengele muhimu vya afya kwa jamii; vilevile panahitajika siasa bora inayojali afya za wananchi.
    Ninavyoelewa mimi Idara ya Afya, pamoja na Idara ya elimu ni sehemu zilizo nyeti sana katika jamii iliyo na upeo wa maendeleo ya jamii zao na nchi yao.
    kwa kusema hivyo sina maana kuwa idara nyingine si nyeti, la hasha.
    Kwa muono wangu, nchi yeyote ile yenye viongozi bora wenye nia nzuri na wananchi wao watazingatia masuala ya maendeleo ya jamii zao na kuzipa idara nilizozitaja hapo juu kipao mbele (afya bora kwa wananchi na elimu muafaka kwa vijana wao).Viongozi hawa watahakikisha kunakuwepo na sera bora ya ufuatiliaji wa shughuli za serekali/maendeleo, na uwajibikaji pale panapotokea uteterekaji katika utendaji.
    Kwa vile najua kuwa mambo ya kiafya siyo ya kuongelea kwenye mitandao au magazetini, ningeomba niishie hapa kwa kuiomba,kuishauri serekali yetu tukufu ijali maombi yote yaliyodaiwa na wataalamu wetu wa afya bila kinyongo chochote.
    Ningeiomba serekali yetu tukufu itafute muafaka haraka wa jambo hili ambalo ni muhimu sana kwa Taifa. Itafute watu watakatifu, wataalamu wa mambo ya afya, wanaoijali nchi yetu na watu wetu wanoishi sasa hivi na vizazi vijavyo ili watutatulie janga hili la afya NOW and FOREVER.
    Migomo ni dalili ya kutokuridhika kwa wanaogoma, hivyo wenye busara wanatakiwa kuchunguza madai ya wagomaji na kuweka kila kitu mezani tiyari kwa majadiliano. Madaktari wa kitanzania sio watu wa kwanza kugoma hapa duniani, migomo ipo toka enzi za industrial revolution, enzi hiyo watu waligoma kupinga uonezi, uburuzwaji na kipato cha chini; hii ni miaka mingi iliyopita huko Ulaya, ni aibu kuwa karne hii ya 21 hili linatokea nchini mwetu na wanaodai haki zao ni watoaji tiba kwa wananchi.
    Swali langu la kiuchokozi ni hili:
    Mbona Wanasheria hatuwaoni wakijigeuzageuza? kulikoni? je wao wanaridhikaje na kipato tukipatacho? au wao wana KEKI ZAO?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...