Kamati ya Redds Miss Tanzania inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.
Shindano la Redd’s Miss Temeke, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya vinywaji vya Redd’s na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com, Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.
Shindano hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.




Huu ndio ujinga ambao WATANZANIA tunauweza, Ovyooo kabisa!Mimi ningekuwa rais ningepiga marufuku upuuzi huu wote maana watu wanakuwa busy for nothing, sasa hapo hao wasichana kwanini wasingekuwa kama kikundi wangeanzisha miradi mbalimbaliya kujiletea kipato na kuliletea TAIFA pato wanachokijua ni kuonyesha mapaja tu! Na vilevile ningekuwa rais MAGAZETI YOTE YA UDAKU NA MENGINEYO yanayochochea chuki na jazba ningeyafungilia mbali ningewaachia GAZETI LA UHURU, MZALENDO,MFANYAKAZI,DAILY NEWS, SUNDAY NEWS na jarida moja la CCM tu!Monday to friday hakuna kukaa pub wala contena wote kazi kama hauna hajira lazima utafagia barabara yaani mi nashindwa kumwelewa JK mbona upole kazidisha sana!?Watu wanasema kazi hakuna mbona kazi kibao bongo ?!HUNA AJIRA UTAFANYA COMMUNITY WORK THEN UNALIPWA KIDOOGO NA SERIKALI MPAKA MNYOOKE WOTE!Nchi inahitaji kupandwa miti hiyo,kufagiliwa,mahospitali kusafishwa watu wanapoteza muda tu FIESTA FIESTA upuuzi mtupu!
ReplyDeleteMdau hapo juu umenena watu wanapoteza muda mwingi kwenye starehe.Kutwa fiesta na kuonyesha uzuri.waje waone sie tunavyobeba boksi
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Hongera!
ReplyDeleteMANA and DEVELOPMENT,
Yaani BINAADAMU na MAENDELEO,
Ni muhimu tukafanya mambo kwa misingi ya tija badala ya kupoteza muda kwa mambo ambayo hayaakisi faida wala kuzalisha tija kwa jamii na maendeleo yetu.
Jambo la Muhimu sawa, wameanza vizuri kwa nia ya Kuamshwa mwamko wa Jamii na mojawapo ya Azma za Mashindano haya ya Mamiss ni kuitumikia Jamaai au kufanya mambo yenye faida kwa Jamii huku wahusika 'Mamiss' wakiwa kama kioo cha kuakisi tabia au mwenendo mwema kwa Jamii.
SASA LA MUHIMU KINACHOTAKIWA NI:
1. KUBADILI MWELEKEO WA HAYA MASHINDANO ILI MAMISS WASHINDANE KTK KUITUMIKIA JAMII BADALA YA KUSHINDANA KWA UZURI NA KUKAA MAPAJA WAZI PEKE YAKE.
2.MAMISS WAMSHINDANE KWA KIGEZO CHA KULETETA MAWAZO ENDELEVU YATAKAYOLETA FAIDA KWA JAMII BADALA YA KUTUMIKA MASHINDANO KAMA MADARAJA YA KUWAPA WASHIRIKI UMAARUFU ILI WAWEZE KUTENDA MAMBO NA TABIA HASI KTK JAMII.
3.PANA MENGI YANATUKABILI KTK JAMII NA VITU VYENYE HAMASA KAMA HIVI VINA UMUHIMU MKUBWA KABISA KUBADILISHWA MWELEKEO WAKE KWA UJUMLA ILI UAKISI TIJA BADALA YA UVUNJIFU.