Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dares Salaam wakiandamana kimyakimya kuelekea viwana vya Jangwani ikiwa ni hatua ya kuonyesha hisia zao za kupinga mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia. 
 Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevil Meena akitoa Tamko.

Tamko lililotolewa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevil Meena, 
kuhusu maandamano hayo.

"Kuna watu wanahoji tunaandamana alafu iweje wakati siye ndio wenye vyombo vya habari si tuandike tu? Hapana kuandamana kwetu kunamaana sana tumeandamana si kama hatuna uwezo wakufanya kitu zaidi ya kuandamana, tunazo silaha kubwa zaidi ya maandamano lakini hii ni hatua ya pili baada ya matamko mbalimbali kutolewa.

Aidha Meena akahoji hivyo inakuaje kama siku moja watu wakaamka wakakuta hakuna chombo chochote cha habari kilicho hewani hakuna tv, hakuna radio na wala hakuna magazeti nchi hii itakuwaje?

Wanahabari waendelee kuwa na utulivu hatua mbalimbali zitakazoendelea kuchukuliwa watafahamishwa kuhusiana na tukio hilo."

Viongozi wengi wa vyama vya waandishi wa habari waliotoa maoni yao kwenye mkusanyiko huo waliitaka serikali wachukue hatua na damu ya Mwangosi iwe shule kwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Swafiii sana waandishi na kuweni kitu kimoja kwani ktk msafara wa MAMBA na KENGE wapo pia. nafikiri mnanielewa

    ReplyDelete
  2. Mmhhhhhhhh!!!!!!!!!! Sasa usiiweke hii maana nyinyi mnataka muungwe mkono tu hamtaki critics

    ReplyDelete
  3. Duh Poleni Ila pia mgewakumbuka na wadau wengine wa mtafaruku huu kwani Nao nani atawawakilishia machungu ya uonevu dhidi yao! wa arusha , moro na k nk

    ReplyDelete

  4. Nami natoa pole kwa ndugu na jamaa, na watanzania wote kwa kifo cha huyo shujaa wa habari.
    Nategemea Waandishi pia mtaacha kuchochea na kutangaza hisia zenu binafsi, badala ya HABARI au MATUKIO ya KWELI.

    ReplyDelete
  5. Si mnasema Tanzania sijui kuna demokrasia, njooni mjenge nchi n.k.

    Nchi bado serikali hawajui demokrasia ni nini. Polisi wenu ni maneno tu katika hotuba mbalimbali wakubwa wao wanahudhuria. Lakini, ukweli ni kuwa bado wanawaonea wananchi. Ukitaka kujua mwananchi wa hali ya chini anaonewa, nenda mahakamani yoyote Dar. Mtu ameiba kitu kidogo, lakini amefungwa miaka 10, kila mwezi kesi inapewa kalenda.

    Mimi nimefika ughaibuni, sijudi kata kwa nini huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...