Ankal na wadau,

Hio hapo ni  website ya Tume ya Uchaguzi ya Angola. Mayokeo yao huwekwa kwenye tovuti yao kadiri yanavyopatikana hivyo kurahisisha vyombo vya habari na wananchi kufuatilia matokeo kadiri yanavyojitokeza. Kutokana na matumizi makubwa ya teknolojia katika zoezi la uchaguzi ikiwemo kadi za kupigia kura za kielekteoniki, taarifa za vituo vya kupiga kura kupatikana kwenye mtandao wa simu, wananchi wa Angola hawalazimiki kuhangaika kutafuta vituo vya kupigia kura, na kushinda vituoni kusubiria matokeo. 

Aidha, tabia ya wananchi wa Angola ni kujihimu kupiga kura na kuendelea na shughuli zao za maendeleo kiasi kwamba ifikapo saa tano mchana vituo huwa ni vitupu. Aidha, utamaduni wa hapa ni kwa wananchi kupiga kura  na kurejea nyumbani kwao na sio kukaa mita mia mbili kusubiria matokeo.


Mdau wa Globu ya Jamii, Luanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...