Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akimtwisha ndoo ya Maji, Bi. Hadija
ambae ni mkazi wa mtaa wa Kilimo aliyoyachota kutoka
katika kisima alichokikabidhi kwa wakazi wa mtaa huo leo.
Mh. Jerry Silaa akimkabidhi seti ya vifaa vya michezo, mmoja kati ya
manahodha wa timu zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu katika kata ya
Gongo la Mboto ijulikanayo kama Jerry Super 8.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni diwani wa kata ya
Gongo la Mboto akizindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa
ushirikiano wake na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilimo Bw. Moshi
Mwaluko.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Gongo la Mboto wakimsikiliza kwa makini
Diwani wa kata yao Mh. Jerry Silaa (hayupo pichani), wakati akiwakabidhi
vifaa vya michezo pamoja na kisima cha maji.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...