Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyeshwa picha ya mfano wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila kabla ya kuanza kwa Harambee ya Kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.Katika harambee hilo iliyoongozwa na Mh. Lowassa,jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada ya Ibada ya Jumapili na baadae kuendeshwa kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mkono na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Robert Mboma, baada ya kuchangia katika Harambee ya Ujenzi wa kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach,Jijini Dar es Salaam,uliofanyika leo.,jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa katika Harambee hiyo.
Meneja wa Kilaji cha Kilimanjaro kutoka TBL, Bw. George Kavishe, akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada kuchangia katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.
BOFYA HAPA AU HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU HAPA KUONA PICHA ZAIDI






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...