
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi jana,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa,alipokitembelea Kituo cha Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi jana,baada ya kufanya ufunguzi rasmi wa kituo hicho kilichojengwa na jeshi hilo,(katikati) Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi Seif Iddi.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Wateja,Mussa Ramadhan Haji,kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji (ZAWA) ikiwa ni miongoni waliochagia katika ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi,wakati wa hafla ya ufunguzi wa kituo hicho jana.

Baadhi ya Maofisa mbali mbali wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Polisi Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana

Baadhi ya Maofisa mbali mbali wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Polisi Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...