Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuviomba  vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge hilo.

 Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga  ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu  tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya nchi tano wanachama wa jumuia hiyo . Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya. 
 
 Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Tasilimu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki  ambao wataufanyia kazi katika kikao cha  Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.


Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki  Abdullah Mwinyi akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa uwanja wa Ndege unaoendelea huko Taveta nchini Kenya kwamba hauna dhamira ya kuathiri uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Kulia ni Katibu  wa Wabunge hao  Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji .

Katibu  wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji (kulia) akiongea jambo na  Abdullah Mwinyi (kushoto) ambaye ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bwana Kimbisa, tell us the role of these MPS. We never voted for them, it is just a heavy burden on the taxpayers. How do you manage 3 jobs if you actually do them efficiently and effectively - CCM NEC, MP, Red Cross?

    ReplyDelete
  2. Wee mdau au tuchague wabunge wa chadema ndio utaridhika, subiri kama mtapata madaraka ndio mtakuwa na nafasi hizi za kuweka watu wenu, hawa waabunge wanatuwakilisha kwenye bunge la EA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...