Kaka,
Pole sana na kaz, tena kwa majukumu.
Kwa majina naitwa mzee Christopher Waru Waga mkaazi wa kijiji cha Bukama wilaya ya Rorya. Kwa kweli ndugu tunapata taabu kubwa ya kukosa umeme kwa zaidi ya miaka 19 sasa tangu nyaya za umeme zipite hapa kuelekea Shirati.Kero hili limeshaongelewa kwa mda sasa na kama kawaida limekuwa kipengele moja muhimu kila mara uchaguzi ufikapo na wengi wamelitumia vilivyo.Tumeona sisi ndio tunaoumia na hivyo basi tumeandaa wenyewe ombi(Page 1 - 5) ambalo tunalisambaza kwa vyombo mbali mbali tukiwa na imani kwamba itamfikia mmoja aliye na uwezo wa kutusaidia.

Linalohitajika ni transformer tu kwani umeme umepita barabarani tu na sisi tunabaki tukiangalia kwa macho na kupeleka simu kijiji jirani kuchaji simu zetu.Tunaomba msaada wako na wanaglobu kwa jumla. Kwa wanaotoka huku kwetu wanajua tunachokiongea.

Tunaomba ombo hili liwafikie wakuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, viongozi wetu pamoja na mbunge wetu Lameck Airo na wadau wote wa maendeleo ya jamii.
Ombi linaelezea zaidi hili tatizo letu.
Shukran sana kaka na Mungu akuzidie kwa kazi nzuri unayoifanya kuiendeleza jamii na taifa letu la Tanzania.
Mungu akubariki.

Kwa mawasiliano:

Christopher Waru Waga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Umeme wa Nini?
    Kodi hata hamjalipa

    ReplyDelete
  2. ndugu maina ang'ela owino njoo nyumbani rorya usaidiana na wananchi tufike mandeleo ya haraka hata kwa chadima. marekani sasa imetosa ukaa.

    odoyo okongo
    wa ingri juu.

    ReplyDelete
  3. jamani yaani miji ya Ruwanda wananchi wake wanataka umeme kwetu bongo?huko huko kweni.

    ReplyDelete
  4. Umeme wa nini Rorya?

    Akina Omera ninyi ni Wasanii wakubwa na kama anavyosema Mdau wa kwanza (kwa kazi zenu za usanii hasa kuchonga mihuri) Kodi hamjalipa kuchangia maendeleo ya nchi.

    Tutawabughudhi wanyama pori ambao ndio wanaochangia mapato makubwa ktk pato la Taifa kupitia Utalii!

    ReplyDelete
  5. WAMASAI WAKIONA BOMBA LA MAJI LIMEPITA WANAPOISHI, HALAFU WAO HAWAJAPEWA MAJI KWA AJILI YA MATUMIZI BINADAMU NA MIFUGO, WANACHOKIFANYA NI KUPASUA BOMBA LA MAJI ILI WAPATE MAJI. ILI KUONDOKANA NA USUMBUFU KWA KUKARABATI BOMBA MARA KWA MARA MAMLAKA HUSIKA HUAMUA KUWAPELEKEA MAJI WAMASAI

    SASA NINYI UMEME UMEPITA JUU YA MAPAA YA NYUMBA ZENU. KILA SIKU MNAAHIDIWA LAKINI HAMPATI UMEME. TAFAKARINI NA MCHUKUE HATUA. NCHI HII USAWA HAUPO KABISA. HAIWEZEKANI NGUZO NA NYAYA ZA UMEME ZIPITE NYUMBANI KWAKO, HALAFU WEWE UKOSE UMEME WAKATI UNAUHITAJI. YAANI UNAACHA UMEME UWANJANI HALAFU UNAKWENDA KUFUATA UMEME KIJIJI CHA JIRANI. DUH POLENI KWA KUTABIKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...