Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten kituo cha Iringa,Marehemu Daud Mwangosi,Afande Pasificus Cleophace Simoni mwenye nambari za jeshi G2573 (kushoto aliejifunika kitambaa kichwani) akifikishwa mahakamani leo kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Mtuhumiwa alijifunika kwa kofia akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi wenzake.Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa mahakamani.
mwandishi maalum wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Iringa anaripoti kuwa ,Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Michael Luena, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.
Amesema mtuhumiwa huyo mnamo Septemba 02 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.
Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.
Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuziba uso kuhakikisha kuwa sura yake haionekanai na waandishi hao.
Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili T 320 ARC Toyota Land cruiser GX tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.



Huu sasa ni uonevu, wahusika wakuu (viongozi wa serikali) wamefichwa na kuletwa huyu mwisho wa siku utasikia anaachiwa huru.
ReplyDeleteHayo hapo waandishi fuatilieni kwa karibu, mazingira hayo mnayosimulia ni ya kutatanisha wanataka kufanya kitu ambacho siyo cha kawaida, moja kati ya haya linaweza kufanyika;
ReplyDelete1) Wanaweza wasingizie mtuhumiwa amekufa Mahabusu wakati kumbe wamemtoa na wamemhamisha kituo cha kazi. au
2)Wanaweza kumtorosha na wakasingizia ametoroka na akaendelea na kazi au akaenda nje.au
3)Kesi ikafifishwa tu kiaina na kuiacha(kuitelekeza)halafu basi.
Hivyo ndo maana wanamficha uso na kumsafirisha kwa gari tofauti na wenzake iliwasimjue punde mambo hayo niliyo sema hapo juu yakifanyika asijulikane kwamba ni yuleyule sasa anafanyakazi mtwara kwamfano.
ASANTE ANKAL. HUYU NI MTUHUMIWA BADO SIO MUUAJI. NIMEONA MAGAZETI MENGI WAMESHA MUHUKUMU.
ReplyDeleteNina mashaka na mashitaka ya "kuua kwa kukusudia" wakishindwa kuthibitisha "kukusudia" basi huyu jamaa anakuwa huru kama tulivyoona kwa kesi nyingine zilizohusu askari. Nadhani wameifanya makusudi.
ReplyDelete
ReplyDeletehahaha yale yale ya zombe...kazi kweli kweli
Jamani kwa kila jambo unalofanya kumbuka utatoa hesabu mbele ya Mungu .. hivyo kanyaga Taratibu hapa duniani sio nyumbani.. mbali na hvyo siku hizi malipo ni hapa hapa duniani wala sio mbinguni
Polisi kuja wamemficha ficha ,hiyo naweza kukubaliana nayo, maana kumbuka kwamba ,a person is not guilty until proven.SO... Je ?? na humo ndani ya mahakama ,hakimu atamficha ??? maana humo mahakamni ,Polisi hana nguvu hata chembe ,huo ni ukumbi wa hakimu na hakimu anaweza kumfunga mtu yeyote yule hata Rais wa nchi.Sasa ,ngoma iko hapo ,je ?? wandishi watakapotaka kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya mahakama ,Polisi wataingilia ??? wacha tuiona hiyo kasheshe. ni mimi Ndagalu ngwana Matolo
ReplyDeleteMwekeni uso wazi tumwone binaadamu mwenzetu ambaye ni ISRAILI mtoa roho za watu!
ReplyDeleteBongo kwa SANAA za MAONYESHO tuko mbele sana!!
ReplyDeleteMbona wale mapolisi waliokuwa wanampiga huyo marehemu Mwangosi kabla ya kupuawa hawashitakiwa. ushahidi upo kwe picha kwamba wanashirikiana kumpiga. mbona wao hawashitakiwa?
ReplyDeleteMany people believe the poor man is merely a scapegoat, the real perpetrators are hiding or being hidden behind him.
ReplyDeleteBTW, how can someone be inculpated at the time when the investigation is not over?