Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia) akipata maelezo juu ya uwepo wa maji katika vyanzo vya maji vya Mkoa wa Mtwara kutoka kwa Afisa wa Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini na Bw. Lazaro Msaru wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Bwinji Wilaya ya Masasi kitakachohudumia Wilaya za Masasi na Nachingwea.
Mheshimiwa Mahenge akipata maelezo juu ya mradi wa Masasi na Nachingwea kutoka kwa Mkandarasi wa mradi huo. Mradi unatarajia kuzalisha lita milioni 12 kwa siku, utawanufaisha wananchi wa Wilaya za Masasi na Nachingwea unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2012 na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Wilaya hizo.
Wananchi wanaokaa karibu na chanzo cha maji cha Mitema, Wilaya ya Newala wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maji (katikati), alipokuwa akijibu kero zao za maji walizoziwasilisha kwake wakati alipotembelea chanzo hicho kwenye ziara yake ya siku 3 Mkoa wa Mtwara huku akishuhudiwa na Mhandisi wa Maji Mkoa wa Mtwara Cosmas Komba (kushoto) na Meneja wa Mamlaka ya Maji Makonde Bw. Mandemla.
Naibu Waziri wa Maji (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika kituo cha uzalishaji maji cha Mtawanya ambacho kinahudumia wananchi wa Wilaya ya Mtwara. Wengine kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Wilman K. Ndile na Kaimu Mkurugenzi wa MTUWASA Bw. Kubilu Masunga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...