Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU,
wanatarajiwa kutumbuiza katika maonesho mengine makubwa. Ratiba inaonyesha kuwa jumatano ya 12.09.2012 bendi hiyo itakuwa katika maonyesho mjini Bremerhaven,na Jumamosi 15.09.2012 kikosi kazi cha Ngoma Africa band, kitaupereka mzimu wake wa muziki katika mji maaufu wa Bremen City,kwenye maonyesho makubwa ya biashara ya kiafrika, "AFRIKA-MESSE" yatakayo katika mtaa wa Messe,mjini Bremen,Ujerumani.
Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 na inayoongozwa na mwanamuziki
kamanda Ras Makunja wa FFU,kwa sasa wanashikilia tuzo la kimataifa
"IDA-International Diaspora Award" imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika iliyofanikiwa kuwadatisha akili washabiki wa kimataifa kila kona.
Tafadhali usikose kujipa raha ya muziki wao @ www.ngoma-africa.com
Ungana nao pia @ www.twitter.com/thengomaafrica
vichaa wa kufanya fujo uone,FFU ninawapenda sana,
ReplyDeleteMdau
Linda
Swiss
Hapa Bremen hakuna Mtaa unaoitwa Messe. Messe ni majumba ya kufanyia exhibition. Angalieni facts kabla hamjapeleka watu Bunju.
ReplyDeleteHapa Bremen kuna maonyesho yaitwayo Hanselife (kama sabasaba kwa dar) na moja kati ya kumbi litakuwa na vitu/products mbalimbali toka africa. Na humo ndio watakuwa hao FFU. Mtaa unaitwa Bürgerweide na hall linaitwa AWD Dome
FFU mimi nawasubiri Bremen naomba mniletee zawadi ya Kirungu cha mpingo
ReplyDeleteNinacho kielewa ni kuwa AFRIKA MESSE,itakuapo pale MESSEHALLE 4.1
ReplyDeletena FFU au watoto wa Mbwa aka ngoma Africa band watakua pale jumamosi 15-9-2012 nilinyosikia katika radio funkhaus Europe.
Mdau wa
Jackob University,Bremen
FFU inakuaje tena lile song la Mama Kimwaga linasika upya redio fankhaus Europe,Ujerumani,wakati nilisikiaga kuwa mlishakatiwa chenu na Jimama kimwaga kuwa bifu limekwisha,sasa mbona redio fankhaus europe wanaupiga kila siku kama dawa za homa?
ReplyDeleteLazima muwege na adabu