Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU,
wanatarajiwa kutumbuiza katika maonesho mengine makubwa. Ratiba inaonyesha kuwa jumatano ya 12.09.2012 bendi hiyo itakuwa katika maonyesho mjini Bremerhaven,na Jumamosi  15.09.2012 kikosi kazi cha Ngoma Africa band, kitaupereka mzimu wake wa muziki katika mji maaufu wa Bremen City,kwenye maonyesho makubwa ya biashara ya kiafrika, "AFRIKA-MESSE" yatakayo katika mtaa wa Messe,mjini Bremen,Ujerumani.

Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 na inayoongozwa na mwanamuziki
kamanda Ras Makunja wa FFU,kwa sasa wanashikilia tuzo la kimataifa
"IDA-International Diaspora Award" imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika iliyofanikiwa kuwadatisha akili washabiki wa kimataifa kila kona.
Tafadhali usikose kujipa raha ya muziki wao @ www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. vichaa wa kufanya fujo uone,FFU ninawapenda sana,
    Mdau
    Linda
    Swiss

    ReplyDelete
  2. Hapa Bremen hakuna Mtaa unaoitwa Messe. Messe ni majumba ya kufanyia exhibition. Angalieni facts kabla hamjapeleka watu Bunju.
    Hapa Bremen kuna maonyesho yaitwayo Hanselife (kama sabasaba kwa dar) na moja kati ya kumbi litakuwa na vitu/products mbalimbali toka africa. Na humo ndio watakuwa hao FFU. Mtaa unaitwa Bürgerweide na hall linaitwa AWD Dome

    ReplyDelete
  3. FFU mimi nawasubiri Bremen naomba mniletee zawadi ya Kirungu cha mpingo

    ReplyDelete
  4. Ninacho kielewa ni kuwa AFRIKA MESSE,itakuapo pale MESSEHALLE 4.1
    na FFU au watoto wa Mbwa aka ngoma Africa band watakua pale jumamosi 15-9-2012 nilinyosikia katika radio funkhaus Europe.
    Mdau wa
    Jackob University,Bremen

    ReplyDelete
  5. FFU inakuaje tena lile song la Mama Kimwaga linasika upya redio fankhaus Europe,Ujerumani,wakati nilisikiaga kuwa mlishakatiwa chenu na Jimama kimwaga kuwa bifu limekwisha,sasa mbona redio fankhaus europe wanaupiga kila siku kama dawa za homa?
    Lazima muwege na adabu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...