Mkuu wa shule ya msingi Ilkonere ,Elihuruma Mollel kulia,akipokea moja ya madawati kati ya 80 yaliyotolewa msaada na benki ya NMB na kukabidhiwa na meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini ,Vicky Bishubo mwishoni mwa wiki katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.Siku hiyo NMB ilikabidhi jumla ya madawati 160 kwa shule mbili za msingi ambazo ni Themi Pamoja na Ilkonere msaada huo unathamani ya shilingi milioni 10.
Mwanafunzi wa darasa la nne ,Linda Olariph (11)akimpongeza meneja wa benki ya NMB,vicky Bishubo kwa niaba ya wenzake kama shukrani ya masaada wa madawati 80 katika shule ya msingi ilkonere iliyopo kijiji cha Olmotony wilaya ya Arumeru,msaada ambao benki hiyo pia ilikabidhi kwa shule hiyo.
Meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini,Vick Bishubo (kushoto)akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongela msaada wa madawati 80 yaliyotolewa na benki hiyo kwa shule ya msingi Themi iliyopo manispaa ya jiji la Arusha.
Meneja wa NMB ,Vick Bishubo wa pili kushoto nyuma,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliofika kuupokea msaada wa madawati,wakwanza kushoto ni afisa elimu wa manispaa ya jiji la Arusha,Omari Mkongole kulia kwake ,mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongella anayefuata ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Zebedayo Mollel na Mwenyekiti wa bodi James Matee pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...