Mjomba, Aslaam aleikhum,
Katika kudumisha undugu wa jadi kati ya wananchi wa Tanzania na Malawi, Planet Darts club ya Kalonga (pichani) imetua nchini kwa ziara ya mchezo wa kirafiki wa darts na Wanyambala wa Tukuyu tangu Jumamosi 01/09/2012. Mechi itaanza muda wowote kuanzia saa 2 jioni ya leo.
Wanyambala wapo fiti sana kwa mchezo huo japo wa Malawi nao wamejiandaa vya kutosha kwa wanasema hawatakubali kuchapwa mara mbili kwani mapema Julai mwaka huu walifungwa kwao Kalonga, Wanyambala walipo watembelea.
Leo ni patashik hapa Tukuyu nguo kuchanika.
Matokeo yatatumwa kwa blog yetu mchezo ukimalizika.
Mjomba Juma
Tokyo
Wakigombana ndugu chukua nyavu ukavue samaki!
ReplyDeleteWamalawi huu ndio undugu!
Sio ule mpango wenu kama vile mnaotumiwa na watu kudai kuwa Ziwa nyasa lote ni la kwenu!
Sasa wanandugu Darts mnatoka kwenu Karonga-Malawi mnakuja Tukuyu-Tanzania mchezo tunacheza wote lakini muda wa chakula mnataka wenzenu tusiwe na kitoweo cha samaki?