Mgeni Rasmi katika Mchezo wa Kombe la Hisani kwa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (SMZ),Mh. Juma Hajji Duni (kushoto) akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba,Ally Said Choma baada ya kuinyuka mabao timu ya Super Falcon mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana usiku kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.Katikati ni Meneja Masoko wa Grand Malt,Fimbo Butallah.
 Nahodha wa timu ya Jamhuri,Ally Said Choma akinyanyua Ngao ya Hisani juu baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi,Mh. Hajji Duni (wa tatu kulia).wengine pichani ni toka kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam,Makau wa Rais wa ZFA,Kassum Suleman,Waziri wa Mifugo na Uvuvi (SMZ),Mh. Abdillahi Jihadi Hassan na Meneja Masoko wa Grand Malt,Fimbo Butallah.
Picha ya Pamoja na Mabingwa wa Ngao ya Hisani Zanzibar 2012.
 Mgeni Rasmi katika Mchezo wa Kombe la Hisani kwa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (SMZ),Mh. Juma Hajji Duni akipiga mpira na kudakwa na Nyanda machacha ambaye ni Meneja Masoko wa Grand Malt,Fimbo Butallah ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar.
Beki wa Timu ya Super Falcon,Faki Ali (3) akiwahi kuuzuia mpira uliokuwa ukielekea kwa mshambuliaji wa timu ya Jamhuri,Ally Said Choma (9) wakati wa mchezo wa ngao ya hisani yenye kuashiria uzinduzi rasmi wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar 2012 uliochezwa kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.Timu ya Jamhuri ndio iliibuka kidedea kwa kuwalaza wenzao wa Super Falcon mabao 3-1.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...