Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua
Bwana Deos Khamis Hubert Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania.
Kulingana
na taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 26, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu
umeanza tarehe 21 Septemba, 2012.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
26
Septemba, 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...