Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akifungua Mkutano mkuu wa 18 wa chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Lindi unaofanyika Wilayani Liwale hii leo.
Maafisa Ushirika wa wilaya za mkoa wa Lindi nao wakiwa katika mkutano Mkuu
Wanachama wa chama kikuu cha Ushirika wakisiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Mkutano mkuu wa 18
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuingilia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa pamoja kukataa bei nzuri zinazoletwa na wanunuzi kuhusiana na mauzo ya mazao ikiwa pamoja na kushawishi wanajamii kukataa kuuza mazao yao kwa vyama vya msingi huku wengine wakiwa na maslahi yao kwa kuwanyonya wakulima ili wasipate bei ya juu
Aidha akisoma taarifa katika mkutano huo. Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi.Kilian Kapamba aliwataka wanachama wa chama hicho kubaini mapungufu yaliyojitokeza katika ununuzi wa zao la Ufuta msimu uliopita ikiwa pamoja na bei kuwa kubwa Wakulima waliibiwa kutokana na vipimio visivyothibitisha na kuwapunja wakulima,Vyama vya msingi na ushirika kukosa mapato,Kutopatikana na takwimu sahihi ya uzalishaji na kufuatia hali hizo aliiomba serikali itilie mkazo mfumo wa stakabadhi ghalani kufuatia mafanikio makubwa yanayopatikana tofauti na soko huria
Picha na habari toka kwa mdau..
Abdulaziz video, Liwale


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...