Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye akifungua mashindano ya Redd's Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Ssebo ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo lililofanyika katika hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wametoa zawadi kwa washindi watatu waliopatikana kwa kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima ndani ya Saloon yao. Shindano rasmi la kumsaka Redd's Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe Septemba 14, 2012 katika Ukumbi wa Cassa Complex uliopo Mikocheni, Dar.
 Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.
 Mshiriki namba 3, Nahma Saidi yeye aliambua kuonyesha mambo ya Pwani.
 Mshiriki namba 2, Ester Musa alionyesha kipaji cha kuimba.
 Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi.
 Majaji wa shindano la Redd's Miss Kinondoni Talent Man Maji (kulia) na mwanadada wakifuatilia kwa makini.
 Mshiriki wa Redd's Miss Kinondoni akichora mlima Kilimanjaro.

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wabongo ubunifu zero na hayo mambo ya umiss mnajipakazia umalaya tu tafuteni michezo mingine mshiriki

    wabongo acheni mambo ya watu kachezeni mdundiko mdumange na ngoma nyingine acheni mambo ya wazungu mnatutia aibu sana


    ReplyDelete
  2. hivi kwanini mabinti hawaweki simu kwenye mikoba? au angalau basi zificheni, kila dakika simu viganjani tu haipendezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...