Na.Catherine Sungura.MOHSW
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi
amesema anapitia taasisi zote zilizopo chini ya wizara yake ili
kusikiliza mafanikio na kujua matatizo yanazozikabili taasisi hizo
ili kuweza kuboresha huduma katika sekta ya
afya nchini pamoja na kupanga mipango mizuri katika kuendeleza
taasisi hizo.
Dkt. Mwinyi amesema hayo leo kwenye ziara
yake na kuzungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Liche
Tanzania (TFNC).
“Lazima tujiulize uwepo wa taasisi hii,mwanzoni
taasisi hii ilikuwa inajikita na utapiamlo, kwa sasa kuna magonjwa yasiyo
ya kuambukizwa ,alitaja mfano wa magonjwa haya ni moyo,kisukari na mengineyo
magonjwa haya mapambano yake ni kinga,na wataalamu wa kutoa kinga
ni nyinyi,hivyo masuala ya lishe ni muhimu kabla ya kuanza kuyatibu.
Aidha Dkt. Mwinyi alisema wizara yake ina kila sababu
ya kuyapa kipaumbele masuala ya lishe nchini licha ya ufinyu wa bajeti
wanayoipata, “ipo haja ya kujipanga upya na kufanya kitu cha
ziada ili kupunguza kiwango cha utapiamlo nchini pamoja na upungufu
wa wekundu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa ambapo inachangia
vifo vya akina mama wajawazito nahii inachangia na akina mama wengi
kutokuwa na elimu na mafunzo juu ya lishe na hivyo nchi kuwa nyuma
na kutofikia malengo ya millennia ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito
nchini.
Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi
hiyo Benetict Jeje alisema taasisi yake ina changamoto
ya kuhakikisha kuwa huduma za lishe nchini zinapanuka na kuwafikia wananchi
wengi hasa waishio vijijini , hivyo serikali kuamua kuajiri maafisa
lishe katika halmashauri 106 kati ya 168 na mikoa 11 imefanya
hivyo.
“Lishe ni suala mtambuka na linalogusa maendeleo
ya kijamii, kiuchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla,ushiriki wa sekta
mbalimbali katika kukabliana na changamoto za lishe nchini ni
jambo lisiloepukika”alisema Jeje.
Hata hivyo alisema taasisi yake kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali zimechangia kupunguza kwa kiwango cha utapiamlo nchini
kati ya mwaka 1999 na 2010.Asilimia 16 ya watoto wenye umri chini ya
miaka mitano wana uzito pungufu,asilimia 5 ni wakondefu na asilimia
42 wana udumavu na upungufu wa damu unaathiri asilimia 69 ya watoto
wakati upungufu wa vitamin A ni asilimia 33.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...