Kaka habari,
Pole na kazi na majukumu mengine.
Samahani kaka mimi ni mdau mtanzania halisi na mwanafunzi,leo asubuhi nilikuwa nipo airport kwa ajili ya safari ya kwenda cairo na ndege niliyotakiwa kuondoka nayo ilipangiwa kuondoka 07:20,chakushangaza nimefika hapa uwanjani kwenye kupima mzigo ili nipewe boarding pass jamaa wananiambia nilipe dola 10.
Ambapo walidai ni ongezeko toka TRA na barua wameonyesha ilikuwa wameibandika pale hazina hata mhuri wa mwenyekiti wa mtaa kuonyesha jinsi ilivyo fojari.
Halafu ni aibu kubwa kwa taifa na kama ni ongezeko linafanyikaje mkononi na halipo kwenye documents? Na mimi nilinunua ticket kwa shirika na sina mkataba na serikari wala TRA.
Kama ni ongezeko mie najua linatokea ukiwa unananunua ticket then, nilikataa kulipa nikakaa pembeni baadae wakaniletea ticket nikakataa nikawauliza mmelipwa dola kumi na nani? Hawakujibu.
Ok baadae walinibembeleza nikaona tu acha niondoke ndo vile nasepa na ndege imedelay kwa 30 min.
naomba waanikwe hawa jamaa kwenye libeneke la Globu ya Jamii ili wajirekebishe maana hii ni aibu sana kwa Taifa letu.
NKALANG'ANGO MTANGO


Mdau hiyo ya dola 10 ipo kama umenunua ticket before July 2012.Hata mimi ilinitokea huku UK na wala sio bongo.Nilibook ticket mapema lakini kabla ya kusafiri agent wangu aliniambia kuna ongezeko la tax kwa hiyo nikalipa.
ReplyDeleteMdau anachosema ni kweli, Hilo lilinikuta tar 17/07/2012. Niliambiwa nitoe dola 10 kama airport charges, nikashangaa, nikawaambia wakati nasafiri sikuwa najua kuwa nitapaswa nilipe airport charges hivyo sikuwa nayo, nikawauliza kwa nini hawawasiliani na airline companies ili hizi charges ziishie kwenye airticket fare? , wakangaliana wakasema aahhh huyu alishalipa. Nikajua ilikuwa deal. Nikaachana nao. Kuna jingine pia wandugu bora hilo kidogo. Kuna jamaa pale wa shirika fulani maarufu la ndege Africa wameanzisha tabia ya kukimbia counters zao kabla ya kumaliza muda wa kucheck in, ili mteja akija pale asiondoke wamchukulie kuwa alidelay na hivyo kulipa fine ili aweze kuunganishiwa ndege nyingine. Na hiyo fine haina receipt wala kipande cha karatasi kuonyesha kuwa umelipa fine. Lakini kwa sababu umeachwa na ndege na umechanganyikiwa unataka kuondoka, wakishaprint ticket unakuwa huna muda wa kuanzisha kesi ni kuondoka tu. Hilo lilinikuta pia, nikalipa pound 30 ambayo inaenda kama 75,000Tsh. Nikaunganishiwa nikaondoka. Lakini kimsingi waliondoka counter kabla ya muda wakijua kuna vichwa watakula na kweli walitutafuna kama watatu hivi wakatuunganishia ndege, wakaweka pesa mfukoni. Airport kumechafuka kwa rushwa, hayo ni matukio ya karibuni lakini kuna mengine mengi tu ya huko nyuma. Nashangaa kwa nini panashindikana kama sio mchezo unaohusu wakubwa pia. Nilishawasiliana na vyombo husika lakini unaishia kukatishwa tamaa maana huna ushahidi wa kutosha!!
ReplyDeleteWewe si kwanza kulfanyiwa wizi huo. Kuna mdau alishalalamika huku na watu wakachangia sana lakini bado hakuna hatua iliyochukuliwa ya ama kuuleza umma uhalali wa kodi hiyo ama kuacha kuchangisha wananchi fedha bila sababu yoyote. Na hata kama TRA watathibitisha kuwepo kwa kodi hiyo, mbona hakuna risiti inayotolewa? Kodi hiyo ilipitishwa na bunge la ngapi? Kuna madudu mengi yanafanyika pale Airport ambapo wananchi wanachangishwa fedha bila sababu yoyote na wakaikataa wanatishiwa kutosafiri.
ReplyDeletewewe umeshaondoka bongo achana na story za bongo zitakuumiza kichwa bure hiyo 10$ tuli chajiwa sisi tuliondoka tokea mwezi wa 7 mwanzoni baada ya budjet bungeni wakasema itaanza kuongezwa kwenye ticket sasa kama bado mpka leo duu ulaji wa maana huo usipime yaani piga hesabu kwa siku ndege ngapi na watu wangapi hahahahaha I love My country Tanzania
ReplyDeleteINAITWA KAMATAAAA MWIZIIIIIII WAKINA ZEBEDAYO HAO WEZI KWELI! RISITI HAWANA WANAENDA KUGAWANA HIZO DOLA 10,10 NJAA BWANA BADALA KUFANYA KAZI ZAO WANAFIKIRIA KUWAKAMUA WATU KWA NJIA ZENGINE KAMA WANATAKA KUFANYA DOLA 10 WAFANYE KITU INAVYOTAKIWA MA RISITI AMBAYO BAADAE UNARUDISHIWA PESA YAKO. KAMATA ZEBEDAYO HAOOOOOO.
ReplyDeleteHakuna dhuluma hapo, hiyo ni tozo halali kabisa iliyopitishwa na vyombo husika. Tatizo lako mdau ni uvivu wa kutofuatilia masuala muhimu. Acha kulalama na kula nafasi bure ya blog yetu.
ReplyDeleteyani hao watu ni wezi mimi ni mtz naish uk but ninapo ludi home nasikia hasira sana na tz airport yani TRA WANAOMBA KUONA MABEGI NA WANASHIKA CHUPI ZETU BILA HATA GROVES BUT KUNA SCANNER PALE HAWATAKI KUITUMIA ,WEZI WEZI,KAZI KUBWA RUSWA NAKUOMBA OMBA ,LAST TIME WALINIULIZA WHY NGUO ZAKO ZOTE MPYA ,SO YANI NITOKE ULAYA NA NGUO KUKUUUU MMMM HAIBU TRAAAAAAAAA
ReplyDeleteMimi waliniambia hiyo kodi, nikalipa dola hamsini kwa familia yangu yenye watu watano, kama walinipiga changa la macho basi wajanja wao, hata kama hela hiyo inaenda TRA, angalia nyumba za mabosi wa TRA, alau hata hawa walala hoi wa airport wapate hela ya vitumbua, ndo sadaka hizo.
ReplyDeleteMimi pia nilillipa July wakati naenda USA na tangazo lilikuwa clear kama umenunua ticket kabla ya July. sasa hivi wamebadilisha, Jumamosi wakati nakuja RSA wakataka kuniibia $10 wakati ticket nilinunua August. Kwakweli Tz tunajiharibia uaminifu, maana walichukua kwa mdada wa Kenya. Baada ya mimi kumwelewesha akaenda kudai fedha yake wakampa. Tena hawatoi hata receipt. Wizi mtupu.
ReplyDeletehakuna wewe unayetetea wizi na wewe ni mwizi ile nchiyetu sote kaka. kitu cha kwanza mimi nilinunua ticket kwa kampuni na sina mkataba wowote na serikali wala TRA, kama ni ongezeko kampuni ndio inaniingizia kwenye jumla ya hela ya kununulia ticket sio from no where unaniambia dola kumi nikupe ukitegemea kwa kuwa naenda nje ntaogopa kukusa safari na kukupa unachodai. mkome nyie vibaka tena mkome maana mimi ni mtanzania halali na ninapokuwa nimenunua ticket najuana na kampuni tu zaidi ya hapo hatutaelewana na mtu anayejifanya @ yeye ni TRA. sheria hatuzijui lakini yale mambo tunayoona tupo on the right TRUCK. hutonigusa just try to always do the right things
ReplyDeletenkalan'ango mtango
http://technupdates.blogspot.com
Mwaka 2010 nilikuwa narudi UK na ndege ya asubuhi sana, ticket yangu ilikuwa inaniruhusu kubeba kilo 46 na za mkononi 12, kwasababu sikutaka kurudi na mabegi UK niliamua kuweka vitu vyote kwenye sanduku moja, kilo zikwa 26 ambapo sanduku moja linatakiwa kuwa na kilo 23, ila kama kilo zako hazitimii unaweza kuweka hata kilo 30 kwenye sanduku moja. Jamaa wakaniambia kilo zimezidi hivyo nilipie hizo kilo tatu, nikawaambia mie nimebeba kilo pungufu maana nilitakiwa niwe na kilo 46, pale kiswahili kikawa kigumu, wakaniweka kando, baadae kidogo akatokea jamaa mmoja anajidai ndo boss akanitishia na kujifanya kuongea kiingereza, mie nikawa nasoma Name berge yake, akanishtukia, nilikuwa nasafiri na kenya air ways lakini ticket nilibook klm, nikawaambia nikiachwa na ndege watanirudishia gharama zangu za ticket, wakaogopa na kunipimia mzigo huku wakisema wamenisaidia, nikawaambia sikuwaomba msaada, hawa jamaa wanatia sana aibu jamani khaa! hata kama ni njaa yakwao imezidi.
ReplyDeleteWadau msiwe wajinga, gharama zote zinazohusu usafiri wa anga zinalipiwa kwenye ticket, wao wanajua mgawanyo wao wanavyoufanya, ukichajiwa gharama za air port unaibiwa, watanzania amkeni.
ReplyDeleteDah Mdau wa UK ndugu yangu sikuvunjii heshima ila jifunze Lugha zote mbili Kiengereza na Kiswahili R na L zimekupiga chenga zinafanya ulichoandika maana yake ni kitu kengine kabisa.
ReplyDeleteWa-Tanzania hiyo Kodi ipo ila bahati mbaya Uwanja wa Ndege Rushwa Kubwa sana hayo Mambo yanataka Elimu kubwa kwenye TV na Radio kujuwa Uhalali wake.
Mdau wa UK Kiswahili na Kiengereza jifunze vizuri L na R zinakupa tabu nakurekebisha kwa heshima tu.
ReplyDeletehahah we mdau wa U.K kama unajua unakuja na mizigo mingi bora ushukie Nairobi mbona watu wengi siku hizi wanafanya hvyo yaani hawataki shida kabisaaa na TRA JNIA ukipita namanga wala hawana shida kama hao wa aiport
ReplyDelete