
Msanii wa filamu nchini almaarufu kama Mtitu akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo AMVCA zilizoanishwa na Africa Magic kwa kushirikiana na Multichoice kwa ajili ya kutambua mchango wa wasanii wa bara la Afrika kwa lengo la kukuza sekta ya filamu Kimataifa.

Wasanii wa filamu wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Tanzania na Afrika kwa Ujumla aliyefariki dunia ghafla Marehemu Steven Kanumba.

Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akiwasisitiza wasanii na watengenezaji wa filamu kuhakikisha zinakuwa na maudhui ya Kiafrika na ubora unaokubalika.Bw. Mwakifamba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda filamu za nyumbani na kushiriki katika kuzipigia kura pindi zinapokuwa katika mashindano ya aina mbalimbali kama itakavyokuwa katika Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA).

Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper Muthamia akielezea kuwa taarifa zaidi kuhusiana na tuzo hizo zinapatikana katika tovuti ya Africa Magic ambayo ni www.africamagic.tv na kuwa kiingilio cha kushiriki katika tuzo hizo ni bure na mwisho wa kuwasilisha fomu za ushiriki ni Oktoba 31, 2012. Kulia ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu.


Risper, you have won my heart, so hot baby!
ReplyDelete