Home
Unlabelled
BINTI ATOWEKA NYUMBANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
WEWEEEEEE...BINTI KAMA HUYU HAWEZI KUTOWEKA HATA SIKU MOJA!!!!!!
ReplyDeleteHahahaha mmumupigwa BAO tayari zamaaaani!
ReplyDeleteMtoto kapata mume!,
Inaonekana Wazazi mlikuwa mmempangia binti kuolewa na Tajiri na Msomi kitu ambacho yeye Binti ameona itakuwa ni pata potea akamwona Msela mmoja ana Genge lake linalozungusha vizuri mauzo na faida na anajitambua na kujiheshimu akaona akaanze nae maisha mapya ya Unyumba!
Mlikuwa mnamfungia Getini huku akiwa mtu mzima na amekuwa na amepata upenyo na sasa anakandamizwa hukooo!
ReplyDeleteYu bukheri wa afya,
ReplyDeleteMsiwe na wasiwasi atakuwa amepata bwana!
Ana miaka mingapi??anaonekana anajua anachokifanya..pole yenu wazazi.kulea kazi sana hasa watoto wakifikia such age
ReplyDeleteMtu mzima anapotea?
ReplyDeleteNijuavyo mimi anatafutwa mtu kwa utaratibu wa RB ya Pilisi kama ametoweka mtu wa chini ya miaka 18 !
Sasa huyu msichana mkubwa na hisia zake timamu za kimapenzi anatafutwa?
Msihara haya jamani..
ReplyDeleteKimwana kama huyu atakuwa "kahifadhiwa mahala"..
Akichoka atarudi tu mwenyewe
Poleni sana mliofikwa na tatizo hili la kupotelewa na binti yenu mpendwa. Labda niulize, huyu sio yule binti aliye katika matangazo ya Silver Botique? Hii itasaidia watu kumtambua kama wakimuona mahali. Tunaomba mtujuze ili kurahisisha kumtafuta
ReplyDeleteAmetoka huyo. Atrudi tu.
ReplyDeleteMtu mzima hatoweki 'anatoka'.
Tena nyumbani? bora ingekua kazini.
poleni wazazi ila hadi zawadi itoke kwa mtu mzima hivi kuna namna ndani ya familia
ReplyDeleteKafichwaaaaaa !!!
ReplyDeleteHaya ndio matokeo ya kuwafugnia Mabinti na kutarajia kuwaozesha kwa Matajiri na Wasomi.
ReplyDeleteMtoto kaona isiwe tabu asijiendee kwa Msela?
jamani huyu mbona ni mtu mzima kabisa..au ni mgonjwa?au ana matatizo au mgeni?
ReplyDeleteotherwise mmeamua kumuabisha kama sio mgonjwa au sio mgeni...
poleni sana...
Sista duu ameona anacheleweshwa na Familia yenye mashariti mengi ameona amuwahi mtarajiwa wake kabla hajakuja kujitambulsha nyumbani!
ReplyDeleteHaya ni makosa mengi familia zetu zinafanya ktk malezi hasa kufikia umri wa aina hii.
Wazazi wanachukulia tabia ya kuwafuga mabinti kama vile hakuna maisha ya baadae ya wao kupata wenza wakaanze maisha mapya, matokeo yake inakuwa kama hapa Binti anaamua kutoroka nyumbani.
Neema ni mtu mzima sasa, je familia mmeshawahi kusema naye angalau kidogo kuhusu matarajio yake ya baadae kimahusiano?
Binti anapofikia umri huu ni vema mkaanza kuwa na ukaribu naye na mkazungumza naye wazi wazi kwa undani kuhusu masuala yake binafsi badala ya kumchukulia kama mtoto mdogo.
ReplyDeleteHivyo ndio tutajenga badala ya kuacha yakatokea ya kutokea kama haya.
Poleni sana!
Mmeangalia chumbani kwake??Kaangalie vizuri chumbani kwake atakuwa ameacha Kitenge cha mama na Jembe....mkivikuta subirini siku 7 'waliomtorosha' watakuja kujitambulisha;..Haaaa haaaaa
ReplyDeleteHuyu ni mtu mzima, sasa ametoweka au kaondoka? Kutoweka ni kama kupotea!!!
ReplyDeletetatizo ni nyie watu wa ughaibuni,mmemrubuni na viwalo vyenu, cha moto mnakiona mnapooa wazungu sasa mnakuja bongo kujichukulia tu badala ya kufuata taratibu za kuposa na kutoa mahali,ngombe au pesa.Kumbukeni kwamba wazazi wamemlea tangia akijikojolea ,sasa kawa mtu mzima !! kwa nini wazazi wasivune jasho lao ??? make sense no ???? zebedayo msema kweli ( ndani ya bongoland)
ReplyDeleteHakuna mtoto mtu mzima kwa mzazi.Mbona Ulaya na Merikani wazazi wana tumia matangazo kutafuta binti aliyo potea au kakimbia nyumbani. Tuombe kwamba kuna marafiki wata soma tanganzo na kumarifu Binti anapendwa na wazazi na arundi nyumbani.
ReplyDeleteMzazi anamtafuta mwanae nyinyi mnafanya masihara. Binti ni mtoto kwa wazazi wake hata akiwa miaka 60. Hata wazee wameshatoa taarifa polisi ya kupotea mtoto wao ujue hii ni kesi kubwa. Tujaribu kuwasaidia ili ijulikane kama yupo hai na wazee sio wajinga kutoa taarifa polisi maana kama mtoto wako hajarudi siku nzima hata kama mtu mzima wakati bado anaishi nyumbani lazima watu wajue yuko wapi. Tumsaidie jamani sio kucheka.
ReplyDeleteAnonymous hapo juu huyo binti ndiyo yeye wa kwenye matangazo ya Silver Boutique, jamani Neema nakumbuka enzi za utoto tunaenda wote mafundisho kanisanai Chang'ombe natumaini upo salama, maana dunia ya siku hizi imeharibika tuache masihara huwezi jua amefikwa nanini kuna watu wanateka watu siku hizi , kuuana ni nje nje kwa hiyo tupunguze imani potofu msichana akipotea basi kapotelea kwa wanaume, Mungu awatie nguvu familai ya Rugarabamu.
ReplyDeleteWamesahau kwamba mtoto kwa wazazi hakui hata akiwa mzee
ReplyDeleteAmeenda kuonana na FACEBOOK wake !
ReplyDeleteUmepita muda mrefu sasa wakiwa ktk mahusiano ya online chat kwenye facebook bila kuonana uso kwa uso hivyo Neema ameona ahakikishe kabisa kwa kuonana nae jamaa asije akauziwa mbuzi kwenye gunia!
Ile jamaa Msela kuona mtoto mkali hivi, asalaleee akachukua simu ya binti akaizima na asimfungie ndani?
Binti alienda kumtembelea facebook wake Msela mmoja hivi akamkuta mgonjwa akaamua aende naye Kijijini kwao jamaa Mkoani kumuuguza kwa Mganga wa Kienyeji!
ReplyDeleteKama anavyosema hapo juu Mdau wa 23 Anonymous wa Wed Oct 24, 10:14:00 AM 2012
ReplyDeleteMabinti muwe makini na marafiki wa mara ya kwanza ingawa tukio hilo sio halisi ni mfano wake.
Hebu angalia unamtembelea mtu ambaye mnafahamiana kwa njia kama ya facebook hamjaonana kwa sura, humuelewi undani wake, unaamua kumtembelea unafika kwake anachukua simu yako anaizima, anaiweka ndani ya droo la kabati lake anaifungia na wewe mwenyewe anakufungia ndani kwake chumbani!
Je, unamwamini vipi huyo mtu?
Una usalama gani na hali yako kwake?
Wasichana muwe makini Dunia sasa imebadilika pana biashara ya viungo vya binaadamu, na biashara za Kiuchawi uchawi!
Wala hawapo mbali!
ReplyDeleteFanyeni kama mnashitukiza vile?
Nyie nendeni hapo Kigamboni kwenye ma Hoteli yale ama Zanzibar Mahotelini huko mtawakuta yeye binti na msela wamepakatana!
Comments za kibongo hazina hofu za mtu kuuawa ama kutekwa kama ilivyo nchi zilizoendelea. Hatuwezi kuhisi labda kapata ajali eneo lisilo na msaada-polini nk.
ReplyDeleteNa kwakuwa si kitu common watu wanaona ni jokes na bla bla. Kumbuka siku itakutokea wewe kwa kupotelewa na nduguyo na hutoweza kuandika pumba zozote.
Tuombeeni usalama wa huyo binnti na faraja kwa familia yake.
Tangulizeni upendo na si vicheko, udaku na pumba.
KWA KIFUPI NEEMA YUPO HAI NA ANAENDELEA NA HALI YAKE VIZURI ILA KIKUBWA KINACHOENDELEA NI KWAMBA HUYO ALIYETOA HILO TANGAZO HAELEWANI VIZURI NA NEEMA-USIPOLIJUA JAMBO NI SAWA NA USIKU WA GIZA.
ReplyDelete