Hiki kibanda kipo pembeni ya barabara ya Morogoro Road maeneo ya Kibamba...nini tafsiri yake?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hiyo tafsiri yake ni Ushindani wa Kisiasa:

    Isipokuwa mambo haya muhimu matano (5) yanahitajika kuzingatiwa ili kufikia lengo kama Tafsiri hiyo niliyoona inavyo kusudiwa,

    1.Siasa ziendeshwe kwa Tija na sio kwa Jazba.

    2.Pawe na Ustaarabu ktk uenezi wa Kisiasa.

    3.Upinzani wa Kisiasa sio Uvunjaji wa Sheria.

    4.Maana ya Siasa sio mgawanyiko kwa Misingi ya Itikadi za utofauti wa vyama na Misimamo ila ni kuleta Maendeleo na kutumia utaratibu huru wa kupata Uongozi unaokubalika na wengi.

    5.Siasa ni Ustaarabu na sio Uadui, Visasi na chuki.

    ReplyDelete
  2. Tafsiri yake mwenye CCM anauza sana Bizaa zake sijui anakopesha yeye? Bizaa zake zina kwisha ila wa Chadema bado Bizaa zimemjalia, au yeye anafanya bidii akiuza tu analeta tena? Sizani sio muuzaji mzuri.

    ReplyDelete
  3. Hiyo Pemba haiwezekani sijui kwa nini? Wapemba wanataka bendera moja tu ya CUF.

    ReplyDelete
  4. Tafsiri yake ni hii: 'Hapa ngoma inogile, mwaga ugali nimwage mboga, nikanyage bahati mbaya nikukong'oli makusudi'

    ReplyDelete
  5. Tafsiri yake ni Kidumbe dumbe chariya mkojozi ka kojowa na nguo kati ya moto.

    ReplyDelete
  6. amenichekesha sana mdau wa mwisho kanikumbusha utotoni laki kidogo spelling kakosea lakini poa ile mbaya hii nyimbo tulikuwa tunaibiwa tukikojoa kitandani duu poa ile mbay michu thanks man kwa kiweka hii comment ya mdau wa mwisho kanifurahisa kiyama

    ReplyDelete
  7. Tafsiri: Tutofautiane ki-itikadi kama kulivyo ndoa baina ya watu wa imani Islamu na Christu na wanajifunika shuka moja wakilala! kama hawa walivyo katika banda moja wakutafuta kuendesha maisha. Hivyo basi; na tudumishe kwa amani na upendo baina yetu.

    ReplyDelete
  8. Bendera hufuata upepo... atakaeshinda huyo huyo ndio nimemchagua... Niachieni biashara yangu iendelee..

    ReplyDelete
  9. huku nipo na huku nipo, atakae boresha mtaji wangu ndie nitakae muelewa zaidi kwa wakati huo wa uboreshaji!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...