Katika Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mahesabu za Mashirika ya UMMA (POAC) mnamo tarehe 24/10/2012 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani K. Dau akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge alitoa maelezo ya msingi kuhusu umuhimu na dhana kamili ya Hifadhi ya Jamii.
Katika maelezo hayo alifafanua kuhusu madhara ya kujitoa kwenye mfuko kwa mwanachama aliye na uwezo wa kuendelea na kazi, na alisisitiza kuwa madhara ni kwa Mwanachama zaidi kuliko kwa Mfuko. Dkt.Dau alifafanua kuwa uamuzi wa kusitisha kwa Mafao ya kujitoa hauna uhusiano wowote na hali ya sasa ya kifedha ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Dkt. Dau aliieleza Kamati ya Bunge kuwa hali ya kifedha ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hupimwa kwa kufanya Actuarial Valuation. Kwa upande wa NSSF zoezi hilo limefanywa mwaka 2009 na Kampuni kutoka Canada iliyoteuliwa na ILO na mwaka 2010 na Kampuni kutoka Afrika Kusini iliyoteuliwa na SSRA.
Matokeo yameonyesha kuwa NSSF HAINA MATATIZO YA KIFEDHA kwa sababu ina uwezo wa kuwalipa Wanachama wake na kulipia gharama za uendeshaji kwa kipindi cha miaka 50 ijayo bila kutetereka.
Dkt. Dau alifafanua zaidi kuhusu kutokuwepo kwa mafao ya kujitoa katika mfumo mzima wa Pensheni ulimwenguni kwa muongozo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) namba 102 wa mwaka 1952 [The ILO Social Security (Minimum Standards) Convention, 1952 No. 102] ambao ndio unatoa maelekezo ya jumla kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii ulimwenguni kote.
Katika Muongozo huu ILO imetamka wazi kuwa kuna aina tisa (9) za mafao yanayotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na katika hayo hakuna mafao ya kujitoa. HITIMISHO Tunapenda kuwataarifu Wanachama na Wananchi kwa ujumla kuwa majibu haya ndio yaliyotolewa katika Kamati ya Bunge.
Taarifa zilizotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari kuwa “Mkurugenzi Mkuu wa NSSF apinga Mafao ya Kujitoa” zimetolewa nje ya maudhui yaani “Out of Context” Suala la Mafao ya kujitoa (Withdrawal Benefit) linashughulikiwa na Serikali na iwapo itaamuliwa na Bunge kurudisha mafao hayo,
NSSF HAINA PINGAMIZI na uamuzi huo na italipa mafao hayo bila wasiwasi wowote kwani ina uwezo mkubwa wa kifedha.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO - NSSF


SISI TUNAFAHAMU KUNA BAADHI YA WATU KWA SASABU ZAO BINAFSI WANAVIZIA NAFASI JAPO NDOGO ZA KUMCHAFULIA JINA MKURUGENZI NSSF. MAJARIBIO YAMEKUWA MENGI NA HILI NI MOJAWAPO.
ReplyDeleteJAMAA ZAO WANAPOFANYA MADUDU WAO AMA HUKAA KIMYA AU HUWATETEA. UBAGUZI NA UBINAFSI UMEWATAWALA, NA NDIO SABABU KUU MASHIRIKA MENGI HUKO TZ HAYAWEZI KUNG'ARA KAMA NSSF.
INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU ATAMLINDA MKURUGENZI WETU NA KUMWEPUSHA NA SHARI NA KIJICHO.
SISI WASWAHILI TUNATOKA KIFUA MBELE NA KUMSHUKURU ALLAH KWA KAZI NA JUHUDI ZA DOKTOR. HE IS THE MAN FOR HIS JOB, WAMEUA MASHIRIKA MENGI KUTOKANA NA UBINAFSI, SASA WAMEBAKI NA CHOYO NA HUSDA DHIDI YA WALE WALIOPEWA NURU NA ALLAH KAMA DOKTOR.
ILA WASICHOJUA NI KWAMBA SISI TUNAHITAJI KUPEWA NAFASI TU TUONESHE UWEZO TULIOJAALIWA KWANI TUNAO. WAACHANE NA ROHO MBAYA, MATOKEO YA TZ KUENDELEA KUWA MASKINI NI UCHAFU WA ROHO ZAO.
LEO HUYO JAMAA YAO MAGUFULI ANATOKA KIFUA MBELE KUTOKANA NA JUHUDI ZA DOKTOOR NA TIMU NZIMA YA NSSF.
DK DAU USITISHIKE, UNAONGOZWA NA NURU YA ALLAH TAALA.
Mndengereko, Ukerewe
Nilipojiunga na NSSF miaka kadhaa iliyopita nilingia mkataba na mfuko huo lakini leo hii mkataba huo umebadilishwa kinyemela na fao la kujitoa kusitishwa bila mimi kushirikishwa. Hii ni haki? Pia nadhani si sahihi kwa Dk Ramadhani Dau kujaribu kulinganisha mazingira ya mifuko ya hifadhi ya jamii na pensheni ya Tanzania na ile ya nchi nyingine. Kwa mfano, alisema fao la kujitoa halipo katika nchi nyingine jirani kama Kenya. Hii ni kweli, lakini inaonekana Dr Dau hana habari kwamba wafanyakazi wote ambao ni wanachama wa NSSF ya Kenya huchangia kima kimoja tu (uniform rate) cha shilingi za nchi hiyo 200 tu (sawa na shilingi za Kitanzania 3,800) kwa mwezi na mwajiri pia huchangia kiasi kama hicho. Hii inamaanisha kuwa mchango wa kila mwanachama wa NSSF ya Kenya ni sawa na shilingi za Kitanzania 7,600 tu kwa mwezi, lakini hapa kwetu mfanyakazi huchangia asilimia 10 ya mshahara wake kabla ya makato (gross pay) na mwajiri kumchangia kiasi kama hicho. Kwa mfano, mfanyakazi mwenye mshahara kabla ya makato wa shilingi 500,000 huwa na mchango wa shilingi 100,000 kila mwezi. Hizi ni fedha nyingi na si haki kumzuia mfanyakazi asizichukue pindi ajira yake inapokoma kwa sababu yoyote ile. Kama Dr Dau anataka kuiga kila kitu kutoka nje, basi atuletee fao la kutokuwa na ajira (employment benefit) kwa wanachama wa NSSF. Kuwepo kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na pensheni Tanzania kuzingatie mazingira ya Tanzania na si kutoa mifano ya nchi nyingine. Huo muongozo wa ILO ni muongozo tu na si msahafu. Hivi kuna miongozo mingapi ya ILO na mashirika mengine ya kimataifa ambayo imekuwa ikipuuzwa hapa Tanzania? Iweje hili la fao la kujitoa tu ndio lishupaliwe na watawala wetu?
ReplyDeleteHatukatai jitihada tunaziona lakini swali je sehria zote zinazowekwa kimataifa zinafaa kutekelezwa maeneo yote, tunazungumziaje hili suala la context...mfano rahisi sana huwezi linganisha hali anayoishi Mtanzania na raia aliyepo nchi zilizoendelea kama Uingereza. Wao wana unemployment benefits, wana National Health Insurance, City Council houses ambazo kwa mtu mwenye maisha ya chini bila ajila hizi huduma zinamsaidia kuweza kuishi, Je kwa Mtanzania ambaye ametoka kazini atalipia nini kodo ya nyumba, atajitibu vipi kwa muda wote huo akisubiri afike miaka ya kupata fao lake....sio kila maazimio yanayotekelezwa kimataifa yanamnufaisha kila binadamu duniani dio maana nchi pia zina uwez wa kutunga sheria zake! we should think and not take everything offered. Mdau S
ReplyDeleteNakubaliana na mdau hapo juu. Mimi ni Mtanzania ninayeishi Kenya na ni kweli wafanyakazi hapa hukatwa shilingi mia mbili tu za NSSF bila kujali viwango vya mishahara.
ReplyDeleteUzuri wa mfumo huu ni kwamba haumuumizi mfanyakazi na unazingatia maisha yake na mahitaji yake ya sasa na pia pale atakapostaafu lakini Tanzania mtu unachangia pesa chungunzima ambazo huwezi kuzichukua hata pale unapoacha kazi ukiwa na umri wa miaka 25.
NSSF na Dr Dau, wadau hapo juu wamekwisha wajibu vizuri tena kwa kutumia mifano/mifananisho yenu wenyewe. Mimi nionavyo Dr Dau na wakuu wenzako mnataka iwe hivyo ili NSSF ibakiwe na akiba kubwa iwe rahisi kwenu kuzifisadi bila kupigiwa kelele mapema, KAMA MAFAO YA KUJITOA HAYATAATHIRI NSSF KAMA MNAVYODAI BASI SHAURI SERIKALI IYARUDISHE HARAKA SANA KWANI NDICHO WANACHAMA WENGI WANACHOTAKA NA MWANACHAMA ASIETAKA KUJITOA PIA ANAWEZA ASIJITOE.
ReplyDeleteKwa nini wabunge wanapewa mafao yao, fedha nyingi kuliko wavuja jasho ambao walikuwa vibarua kwenye mashirika, leo wananyimwa hata kile kidogo ambacho wangepewa hii sio sawa.
ReplyDelete