MKUU wa Shirika la Kitawa la Consolata la Kanisa Katoliki nchini, Padri Salutaris Massawe (pichani) amefariki Dunia baada ya kuzidiwa na maji ya Bahari wakati akiogelea katika ufukwe wa Pwani ya Bagamoyo Oktoba 25.

Padre huyo ambaye alikuwa yupo Bagamoyo kwa shughuli za shirika lake, alizidiwa na maji hayo ambayo yalimchukua majira ya alasili ya siku hiyo wakati alipokuwa akiogelea pamoja na wageni wa shirika hilo walioitembelea Bagamoyo. 

Mwili wa Marehemu Padri Salutaris Massawe ulipatikana jana asubuhi katika fukwe hiyo ya Bagamoyo.

Akizungumzia tukio hilo mbele ya Ripota Wetu, Katibu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Joseph Masenge alikiri kutokea kwa kifo cha Padri huyo, ambapo padri huyo alifariki baada ya kuchukuliwa na maji alipokuwa akiogelea juzi saa tisa alasiri (kwa saa za Afrika Mashariki) na mwili wake kuonekana jana asubuhi ufukweni.

Padri huyo alikuwa akiogelea baharini karibu na Msalaba Mkuu wa Bagamoyo.

Hadi jana mchana Padri Masenge alisema walikuwa katika maandalizi ya kuusafirisha mwili wa Padri Salutaris Massawe kuja Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuhifadhi wakati mipango ya mazishi ikiandaliwa.

Naye, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Eusebius Nzigirwa alisema kifo cha padri huyo kimeacha pengo kubwa kwani wamepoteza mtu mchapakazi na aliyefanya kazi kwa mipango.

Alisema anamfahamu Padri Massawe kwani aliwahi kufanya kazi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkuu wa shirika hilo ambapo aliwajibika vizuri katika kusimamia majukumu yake.

Alisema kwa taarifa alizozipata awali, Padri huyo alikwenda Bagamoyo na wageni wa shirika ambao walitaka kupata historia ya jinsi Ukristo ulivyoingia nchini pamoja na historia nzima ya ukristo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Apumzike kwa Amani Padri Massawe,
    "....Kuusafirisha mwili wa padri Salutaris Massawe kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili.....kwa ajili ya kuuhifadhi...."

    Vifo kama hivi ni vizuri vifanyiwe uchunguzi kabla ya mazishi, did he have a heart heart attack before drowning? let us not assume that "maji yalimshinda", did he have a previously undiagnosed cardiac condition?

    Surely MNH has some good Pathologists to carry out post mortems,in UK this would be referred to the Coroner and a post mortem is a must in order to find the cause of death.

    All that said, ret in peace Father Massawe.

    ReplyDelete
  2. Ampuzike kwa Amani Padri Massawe.Kwa kweli ni pigo kubwa kuondokewa na Mpendwa sana kaka yetu Padri Massawe. Ni vigumu mno kuyapokea haya. Mioyo imejaa majonzi yasopimika. Tuendelee kumuombea kwa Mungu, na kumwomba Mungu pia atujalie nguvu na uvumilivu katika kipindi kigumu.
    Bwana ametoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe. Pumziko la Milele Umjalie Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie. Apumzike kwa Amani. Amina

    ReplyDelete
  3. Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani. Amani.

    ReplyDelete
  4. Leo nili soma habari kwenye gazeti la HabariLeo lakini siku amini. Mungu amlaze pema.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza hilo si kwa Tanzania kaka,Tanzania ukifa usiku kesho asubuhi ushazikwa, kuna vifo vingi vyenye utata vinatokea ambavyo kulikua na kila sababu ya kufanya uchunguzi kabla ya kuzika lakini wapi.Lakini hili nalo yawezekana likawa linakwazwa na baadhi ya mambo fulani fulani mfano: sheria na taratibu za kidini, ufahamu wa watanznia juu ya suala hili la uchunguzi kutambua sababu za kifo, Umasikini wa fedha za kulipia iwapo utahitaji kufanya uchunguzi, sina hakika kama tuna wataalam wa uhakika wa fani hii kwa tanzania.
    malalamiko na kutoridhika yamejitokeza yenye kuhusisha kifo au vifo vyenye utata viwe vya ghafla au hata visiwe vya ghafla.
    Uchunguzi wa namna hii ni wa manufaa si tu kwa wafiwa bali hata kwa serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...