Dr Ayub Rioba akihutubia muda mfupi baada ya kutunukiwa
shahada ya udaktari wa Falsasa(PhD) katika fani ya Sayansi ya Jamii, Chuo kikuu cha Tampere katika jiji la Tampere, Finland.
Meza kuu kutoka
kushoto Dr Ayub Rioba (University of Dar es salaam, Tanzania) Prof
Kaarle Nordenstreng (University of Tampere, Finland) pamoja na Prof
Audrey Gadzekpo (Accra University, Ghana).DR Rioba akijibu moja ya
maswali kutokana na utafiti wake wa "Media accountability in Tanzania's Multiparty democracy: Does self regulation work?" (picha zote na Paula Paukku)
Kabla ya kula nondo yake alitumia zaidi ya masaa mawili kutetea tafiti yake ya "Media accountability in Tanzania's Multiparty democracy:Does self regulation work?"
Baada ya mjadala mzito wa kitaaluma na maswali kibao ya Prof Audrey Gadzekpo kutoka Chuo kikuu cha Accra, Ghana pamoja jopo la maprofessa walifikia hitimisha na kumtunukia shahada ya Falsafa ya Udakati(PhD) katika fani ya Sayansi ya jamii.
Wadau wanakupongeza kwa hatua hiyo ,na kukutakia kila kheri katika kuitumikia jamii..
Hongera DR AYUB RIOBA!
http://edondaki.
WASIMI UTAWAJUA TU, USO UMETULIA, VERY SERIOUS MAN.HONGERA SANA, INAPENDEZA KUONA NASISI TUNASOMA NA KUFIKA MBELE ZAIDI.HONGERA SANA BABA, SURA YAKO INAONESHA KABISA UNARUDI ZAKO NYUMBANI, NENDA WAACHIE WANA TAMPERE MJI WAO,MAANA JIJI KWA WABEBA BOKSI HILO NI BALAA. IGENI MFANO JAMANI, SIO MNASOMA MNAWEKA VYETI MASANDUKUNI MNAZUNGUKAZUNGUKA TU KWENYE PICNIC NA DISCO ULAYA. KAENI HUKO MKIFANYA YA MAANA, ONGEZENI ELIMU ZAIDI,KASAKI OPPORTUNITIES NCHI ZINGINE KAMA HUKO PANAGOMA AU RUDINI NYUMBANI NA VYETI MLIVYOKWISHAPATA. KUNGOJEA HADI MUWE 50 KUAMKA USINGIZINI ITAKUWA NOMA, MTAKUJA KUUMBUKA.
ReplyDeleteHongera sana Dr.Ayub, nyie ndio mnailetea Tanzania yetu heshima zaidi kila kunapokucha maana kwa mengine nchi inatungusha ila kwa kutoa vichwa kwakweli inafurahisha.Tanzania tuchangamke kuwaheshimu wasomi jamani, tunavyowawekea mazingira magumu ya kazi na maendeleo yao ndio maana wanakimbilia south africa na nje
ReplyDeleteHongera sana ndugu yetu, khaaa umenitia donge, nimesikia wivu maana namimi ni dream yangu hiyo, then nikiwa kama mwanamke i am proud of huyo Mghana na wengine wakina mama wa kibongo waliojitahidi kuinamia kitabu kwa sana. Yaani huyo professor mghana kanitia uchungu ile mbaya, wacha nikakazanie Masters Thesis yangu nimalize namimi nirukie PhD, INSHALAAH
ReplyDeletesafi sana Dr Rioba, now we are talking. hatufahamiani, lakini i'm really proud of your good work.
ReplyDeleteHongera sana Mwalimu wangu Rioba. Nimefurahi sana na nahisi shahada hiyo ni zawadi umetupatia waandishi wa habari wa Tanzania. Tuliopita mikononi mwako katika fani hii naamini kama ilivyo kwangu tunakupongeza kwa dhati. Muhimu Mchango wako katika tasnia hii bado unahitajika kwa kiasi kikubwa hasa wakati huu ambapo changamoto zimeongezeka kiasi cha kutishia heshima mustakabali wa tasnia hii. Mimi nakutakia kila la kheri na usiishie UDSM pita nchi nzima kamanda angalau utaokoa jahazi hili kabla halijazama kabisa. Nimefurahi sana na nakutakia heri nyingi katika safari yako hii ambayo hata hivyo mimi nilitegemea utafika hapo na naamini utaenda mbali zaidi kwa sababu WEWE SIO KIATU.
ReplyDeleteHongera Dr. Ayoub ukirudi bongo una bia zako nimeshakutolea order utazikuta Hongera Bar.
ReplyDeleteMimi sishauri urudi Tanzania kwa sababau kuna anti-intellectualism mentality hapa. Wasomi hawapewi nafasi na wala hawathaminiwi. Huhitaji kwenda mbali jiulize Intelligentsia yetu wako wapi? Hii Tanzania ya 2012 ni ambayo imejaa wazandiki, wanafiki, waliojaa husda na bila kusahau mafisadi.
ReplyDeleteAnayethaminiwa ni mwenye pesa na wezi. Nashauri tafuta kazi nje ya nchi na ikiwezekana chukua uraia wa nje huko utathaminiwa zaidi kuliko nyumbani.
Ukwlei ndio huo japo unauma
Hongera sana Mwanandugu Dakitari Mtunukiwa Ayubu Rioba !!!
ReplyDeletePia hilo somo lako ni muafaka sana kwa kipindi hiki hapa nchini ktk Mchakato wa Habari na Masuala ya Siasa za vyama vingi.
Ahsante sana Dr. Ayubu Rioba !
MATHAYO said...
ReplyDeleteHONGERA SANA MKUU!! WE ARE VERY PROUD AND LOOKING FORWARD TO SEE YOU SOON TO CELEBRATE THIS ACHIEVEMENT, NAONA NI KAMA MIMI NDIYO NIMEKUWA DR...
Halafu walee kina nani hii wanaokwepa umande, walalama kunyanyaswa! Rioba nani kamtuma kusoma? Si pesa yake angeweza olea mke wa nne!
ReplyDelete