Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na
wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara
iliyoanywa na wajumbe hao leo jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012 ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo
katika Makao Makuu ya Tume hiyo Jijiini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi
Chana.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, (kulia) akibadilishana
mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi
Chana (katikati) wakati kamati hiyo iliyofanywa leo jumanne tarehe 16. Oktoba,
2012 na kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika makao makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki.
Katibu
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara ya wajumbe hao iliyofanywa
leo jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012 na kutembela vitengo mbalimbali vilivyopo
katika Makao Makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni wajumbe
wa Kamati hiyo, Rashid Ali Abdalla, Deogratius Ntukamazina, Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Felix Mkosamali
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala wakitazama namna ya Sauti zenye maoni ya wananchi
zinazokusanywa kutoka Mikoa mbalimbali nchini namna zinavyoweza kupokelewa
katika Makao makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Pindi Chana na wa pili kulia ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.
(Picha na Tume ya Katiba)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...