Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Tanzania Limited, Jokate Mwegelo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa lebo yake ya Kidoti kwenye hotel ya Serena.
Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo amezindua rasmi lebo yake ya mitindo ya nywele na nguo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Brand.
Jokate ambaye alianza kujihusisha na masuala ya mitindo mwaka jana, alizindua lebo yake hiyo kwenye hotel ya Serena na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa masuala ya urembo, maonyesho ya mavazi, wanamitindo na wauzaji wa bidhaa hizo kutoka kila kona ya jiji.
Alisema kuwa hatua ya kuamua kuanzisha lebo hiyo ni moja ya mikakati yake ya kujitafutia fedha kama mjasiliamali na lengo lake kubwa ni kutaka kusimama yeye mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu.
Alifafanua kuwa kabla ya kuanzisha lebo na kampuni yake, alifanya utafiti wa hali ya juu, kuhusiana na sekta hiyo na hatimaye kushiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya mavazi ya Red Ribbon na sasa kuamua kwenda mbali zaidi kwa kuingia katika fani ya nywele ambazo anatengeneza yeye mwenyewe.
Amesema kuwa mbali ya kushiriki katika maonyesho mbali mbali, pia atakuwa anasambaza bidhaa zake za nywele na nguo kwenye maduka mbali mbali ili kuwawezesha wananchi kutumia bidhaa zake.
“Lengo langu kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea, hiyo ndiyo ndoto yangu pamoja na kuuza bidhaa zangu hasa za nywele kuanzia shs 9,500 na 12,000.
Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi,” alisema Jokate.
Alisema kuwa msingi wa ubunifu wake ni mchanganyiko wa kipekee wa kiini cha utamaduni wa Kiafrika pamoja na mitindo ya kisasa ulimwenguni kwa ajili ya wanawake na wanaume wa kisasa.
Wanamitindo wakionyesha staili tofauti za nywele zilizo tengenezwa na Jokate


How on earth can we bring sense onto girls that Natural is Beautful? This Kidoti is disustrous!
ReplyDeleteAtawini jokate bonge la LOGO hilo akikomaa anakwenda international;atafute watu wa zuri wa graphics watumie kidoti chake au8 sura yake kwa ajili ya t shirt'safi sanaa jokate kazana tayari ushapiga atua1.
ReplyDeletei agree with the fist mdau how on eathd can we bring some sense onto girls that natural beautif is awesome siyo eti kubandikaka mawigi na manyele ya watu walio kufa, jipange kama flavia matata alivyo natural ukitaka watu wawe serious na wewe na biasha yako, utoto achaa mamaa kaa na uzuri wako wa asili ridhika unatazamwana na dunia kila pembe uendayo jicho linakupika na unavyo appear na jinsi ulivyo ndo watakavyo kuchukulia so acha kutiam minyele ya ajabu ajabu au rangi za ajabu ajabu wanao fanya hivi ni walio lost kimaisha. ushauri wa bure joketi because nakupenda unde bele zaidi kimaisha.
ReplyDeletehongera sana jokate na utafika mbali na hii project yako. usikatishwe tamaa na mtu yeyote the sky is the limit
ReplyDeleteNYWELE BANDIA BIASHARA IPO, ILA YAFANYE MANYWELE YAFANANE NA UHALISIA KIDOGO. UKITENGENEZA WIGI ANGALIA MTU MWENYE NATURAL HAIR NZURI HALAFU UIGE. SIO MANYWELE YA KURUNDIKA RANGI ZA AJABU, SOKO UNAMLENGA NANI?
ReplyDeleteNimpende nani, nimpendeee eeeeeeh/ Nimpende nani nimpendeeeee aa aaaaah/
ReplyDeleteLovely brand name and I can guess where it came from, cuuuuuute!
That is a big step Kidoti!Lebo yako ni very unique! Usikatishwe tamaa na mtu! ready the stories of successiful people.They all started on simple ideas like yours. Usikatishwe tamaa na yeyote. Keep i up!
ReplyDeleteWapi "twende kilioni", "Kilimanjaro", "mdomo wa kuku", "mabutu", "vitunguu" NK?
ReplyDeleteHongera sana Jokate wanawake na maendeleo ujumbe mzito kinamama anasema hataki kusubiri vya kupewa anajitegemea mwenyewe hongera sana binti kaza buti hata Bakhresa alianza na kibanda cha icecream utafika na wewe ziba masikio hao wanaokatisha tamaa kama mdau wa kwanza usiwasikilize kabisa angalia mbele
ReplyDelete