Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi leo amepokea Ripoti ya Kamati aliyoiunda mwezi uliopita kupata taarifa kuhusu vurugu zilizotokea Mkoani Iringa ambazo zilisababisha kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Vurugu hizo zilitokea Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.

Akikabidhi Ripoti hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Theophil Makunga alisema Kamati yake ilifanya ziara mkoani Iringa na kufanya mahojiano na wadau mbalimbali na pia jijini Dar es Salaam.

Akipokea Ripoti hiyo, Waziri Nchimbi aliishukuru Kamati hiyo kwa kazi waliyoifanya na kusema yeye na Kamati hiyo watafanya kikao na Waandishi wa habari siku ya Jumanne saa 4 asubuhi.

Imetolewa na  Isaac J. Nantanga
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
06 Sept., 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. iwekeni basi ripoti hapa tuione. kuna usiri gani tena wa kuficha ficha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...