KIJANA MMOJA ALIYESHUKIWA KUWA NI MWIZI AMEPATA KIPIGO KIKALI PALE ALIPOKUTWA AKIIBA WHEEL COVER ZA GARI AINA YA NOAH HUKO MAENEO YA KINONDONI USIKU HUU NA BAADA YA KIPIGO WASAMALIA WEMA WALIMUOKOA KIJANA HUYO NA KUMUACHA HURU HUKU KIJANA HUYO AKIWA HOI NA KUKIMBIA KUSIKO JULIKANA.
WANANCHI WA ENEO LA KINONDONI WAKIENDELEA KUMUADABISHA KIBAKA WALIOMKAMATA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wheel cover au wheel caps?

    ReplyDelete
  2. umeshaelewa wewe anony wa kwanza.unataka kuleta shule hapa.ujumbe uliokusudiwa hapa ni kupigwa kwa kibaka na sii wheel cover au caps.

    wangemuua tu huyo, wanakera sana japo chanzo cha yote haya ni ajira ngumu na zikitokea wanapeana wao kwa wao sisi maskini ambao hatuna ndugu zetu serikalini au wenye wadhifa popote tunakimbilia kuiba..alaumiwe nani-viongozi wa nchi

    ReplyDelete
  3. Duhhh baada ya Msala wa kipigo asubiri mwingine kutoka Ubalozi wa Spain nchini Tanzania kwa kidhalilisha nchi yao!

    Kwa nini?

    Ni vile Kibaka amefanya wizi akiwa amevaa Jezi ya Timu ya Taifa ya Spain ambaye kwa sasa ndiye Bingwa wa Ulaya na Dunia !!!

    ReplyDelete
  4. Uhispania imeshiriki wizi hapa!

    Kibaka ameiangusha sana Uhispania kwa jezi aliyovaa wakati wa wizi.

    Hivi Bandugu hizi Jezi ama Fulana za Timu tunavaa kwa kujua tunawakilisha timu gani?

    ReplyDelete
  5. l think you understood what he ment to say. The meaning doesn't differ that much.

    ReplyDelete
  6. Mtaacha lini kujichukulia sheria mikononi, mkiendelea hivyo hatimae hamtaona shida kuua albino au wenye macho mekundu.

    ReplyDelete
  7. Hahahahaha hii picha itatusababishia maelewano mabaya na Spain baada ya kuona picha ina mchezaji wa Timu yao ya Taifa kwa Jezi akiwa chini, akigombewa kama mpira wa Kona na anapokea kichapo cha Watanzania Kinondoni!

    Vita na Spain tutaiweza mwanawane wakati Malawi inadai ziwa Nyasa bado kamasi zinatutoka?

    ReplyDelete
  8. Italia wana Mchezaji mtu mweusi Mario Balotelli,

    Je bandugu nao Spain mchezaji wao wa Timu ya Taifa mweusi (KIBAKA) huyo anayepigwa aliyevaa jezi ya Spain chini ndio nani ?

    Ni Maganga au Mbonde (mzaliwa wa Tanzania) na mchezaji wa Timu ya Taifa ya Spain?

    ReplyDelete
  9. Alikuwa anahitajika kupelekwa polisi sio mob justice.Bongo hovyo sana.Marehemu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza yeye alikuwa anachota mbona hakuna aliyempiga?

    ReplyDelete
  10. Bwana kaka angalia!

    Wapi ulisikia maisha yanatafutwa kwa kutumia mabavu na kulazimisha kwa wizi?

    Je, mpaka ulazimishe maisha kwa njia ya wizi wa kijinga, hivi ulishajaribu ukashindwa kuyakabili maisha kwa kutumia pia akili na jitihada?

    Wajameni tuache kuyaendelea maisha kwa mti ndo huu tutakwisha!!!

    ReplyDelete
  11. Watu kama hawa ndio wanaotujazia magereza na mabasi ya Mahabusu wakati Mafisadi wanaheshimiwa na kuendelea kutesa na kutamba Mitaani!

    ReplyDelete
  12. Viongozi wezi nao wapewe vichapo kama huyu, maana wanakera sana

    ReplyDelete
  13. ANONYMOUS 2 UTAJUAJE KAMA ANONYMOUS 1 ANAJUA KIMOMBO???? hahahahaha alitaka kuanzisha mjadala mwingineee kabisa na wakati ujumbe umeeleweka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...