Unapopata watoto,upende au usipende, kama mzazi huwa kuna ushawishi fulani binafsi katika taaluma ambayo ungependa waje kufanya. Na hiyo huwa inatokea kwa nia njema tu.Kama mzazi unakuwa umeshaona mengi.Umeshaona kazi ambazo “zinalipa” na ushaona zile ambazo unadhani mwanao ataishia kusiko. Pamoja na hayo,sio wazazi wote hufanikiwa. Kadiri mtoto anavyokua,naye anaona na ana ruhusa ya kufanya anachoamua yeye kufanya.Hali kama hiyo ikitokea,kama mzazi,huna jinsi bali kumuunga mkono kwa mapenzi yote. 

Sasa tukizungumzia Mzazi mmojawapo ambaye amefanikiwa kuwafanya wanawe wapende kile anachokipenda yeye si mwingine bali Mzee Matumla. Kutokana na mapenzi yake kwa mchezo wa ngumi,amefanikiwa kuwafanya wanawe na sasa wajukuu zake,kuupenda na kuucheza mchezo wa masumbwi. Watizame hapa wanawe Hassan,Rashid na Mbwana wakiongea na Salama Jabir,Johnie na Muba katika kipindi cha Mkasi ambacho safari yake huanzia pale Amaya Beauty Salon & Spa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...