Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi akichangia majadiliano ya ajenda namba 27 kuhusu Maendeleo ya Jamii, Kamati ya Tatu ambayo ni Moja ya Kamati sita zinazounda Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa na kama ilivyo kwa kamati nyingine imeanza majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu suala zima la maendeleo ya jamii, ambapo taarifa mbalimbali zimekuwa zikipokelewa na kujadiliwa.
Kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa inapata fursa ya kuelezea mafanikio na changamoto inayokabiliana nazo katika utekelezaji wa jukumu la kuwaletea maendeleo wananchi wake. Aidha wajumbe wamekuwa pia wakitoa mapendekezo na ushauri wa nini kifanyike ili kusukuma mbele ajenga ya maendeleo endelevu na kuupiga vita umaskini kwa njia ya ubia kati ya nchi hizo, Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo. Katika Mkutano huo Tanzania kwa upande wake imesisitiza haja na umuhimu wa watu wenye ulemavu kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo kwa kile inachosema kwamba kuna uhusiano wa karibu kati ya umaskini na ulemavu na kwamba kundi hilo la jamii ni muhimu sana katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs).


Walemavu wanatakiwa wapewe haki zao za kimsingi.
ReplyDeleteUmoja wa mataifa umeshindwa kabisa kutekeleza shughuli zake.Nchi kama Tanzania ni mwanachama na kila siku tunaona walemavu wanavyonyanyasika.Kama nchi ni maskini ilitakiwa umoja wa mataifa usaidie kutoa huduma za kimsingi kwa walemavu.
Mfano kusaidia nchi kujenga vivuko kwenye barabara kubwa ili walemavu wawe wanaepukana na ajali za uzembe.
kuhakikisha walemavu wanapatawa msaada wa lishe ikiwa pamoja na kujengewa makazi ya bei nafuu.
Umoja wa mataifa unashindwa kabisa.
Ulemavu wa akili ndio mbaya zaidi.
ReplyDeleteBinadamu yoyote anahaki za kimsingi awe anaulemavu wa akili n.k
ReplyDeleteWajapan wanaamini anayeona mlemavu wa akili ni tatizo basi yeye ndiyo anaulemavu wa akili zaidi.
Kila kitu kinasababu.Kila sababu inaakisi upande wa pili.