Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kubainika kwa matumizi ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi zenye jina la Biashara TT –VIR 30.
Mmmoja wa maafisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari akiwaonyesha waandishi wa habari Dawa badia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVS) zilizoondolewa katika vituo vya kutolea huduma mara baada ya kugundulika.
Makopo ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi yakitofautiana vifungashio. Kopo la kwanza kushoto linaonyesha dawa halisi ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyokidhi viwango ikifuatiwa na makopo 3 yenye dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi yenye jina la biashara TT –VR 30 toleo namba 0c.01.85 yaliyotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Fuatilieni na TFDA wanaochukua pesa ili dawa fulani ziingie mitaani na wanaokataa kulipa, haziingii wakati ni dawa nzuri kabisa zinazopendwa na madaktari na zinafaa kupona magonjwa

    ReplyDelete
  2. MSD NI CORRUPT SANA...WANA QC NZURI SANA NA WASOMI WAZURI WA MAABARA IMEKUWAJE LEO WAINGIZE DAWA FAKE SOKONI?ITAKUWAJE KWA WAGONJWA AMBAO SASA WATAPATA RESISTANCE NA HATIMAYE KUFA? KUSIMAMISHWA HAITOSHI ILA KU NYONGWA NDIO DAWA SAHIHI!!

    ReplyDelete
  3. Kopo bandia la pili kushoto hata lebo imegeuzwa chini juu, kweli ukishangaa ya MSD utaona ya Tanzania pharmaceutical!

    Pili, bandia kwa maana kuwa dawa bandia haipunguzi makali au wamedesa madawa bila ruhusa ya mwenye patent au ni bandia hazifanyi kazi, ufafanuzi Ankali?

    ReplyDelete
  4. Tanzania Ufisadi Kila nyanja...Baada ya huyo mkurugenzi kutupwa selo eti anapisha uchunguzi huku akiwa Royal palm anakula supu ya Kongoro. Huyo anacheza na roho za watu alafu anapisha uchnguzi badala ya kupisha karandinga na kuingia selo?!! Mi naona Waziri wa Afya Angejiuzulu pia kwa kutofuatilia wizara yake ipasavyo..Tumekwisha jamani daaa

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau namba 4, Waziri huyo atafukuzana na makampuni mangapi na kuangalia dawa gani zinafaa au hazifai?.

    Ndiyo maana kuna akina TFDA ili waweze kuhakikisha hivyo vitu viko sawa.

    ReplyDelete
  6. Wanaotaka kumwangusha Madabida kisiasa wanapitia njia za mkato. Ndio maana Nyerere alikataa kuwa mfanya biashara na kuwa mwana siasa kwa wakati mmoja.
    Sasa hii ni fitna ya wapinzani tu.

    ReplyDelete
  7. Lol, Afisa wa TFDA hakutaka jina lake litajwe halafu yuko kwenye picha!!! and i also see video cameras :)

    $D

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...