Ikiwa imebaki siku moja ili kuanza kwa usafiri wa Treni ndani ya jiji la Dar es Salaam,Wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania (TRL) wameanza kufanya maboresho kwenye reli zote ambazo zitatumiwa na Treni hizo zilizopo maeneo mbali mbali ya jijini Dar.Pichani ni Wafanyakazi hao wakiboresha reli hiyo eneo la Tabata AMI karibu kabisa na zilipo ofisi za uchapishaji wa magazeti ya Mwananchi.
UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA - TRL UNAFURAHA KUWATAARIFU WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA WANANCHI KWA UJUMLA KUWA HUDUMA WALIOKUWA WAKIISUBIRI KWA HAMU ITAANZA SIKU YA JUMATATU OKTOBA 29, 2012.
HATA HIVYO ILI KUPATA HUDUMA HIYO BILA USUMBUFU KUTAKUWEPO WAKATA TIKETI NJE YA KILA KITUO NA HIVYO HAIRUHUSIWI ABIRIA KUINGIA NDANI YA TRENI BILA YA TIKETI. TIKETI KUTOKA DAR STESHENI HADI UBUNGO MAZIWA AU POPOTE KATIKA VITUO SABA NI SHILINGI 400 KWA MTU MZIMA NA SHILINGI 1OO KWA MTOTO .
HUDUMA ZITAANZA KILA SIKU SAA 11 ASUBUHI HADI SAA 5 ASUBUHI NA ALASIRI KUANZIA SAA 9 HADI SAA MBILI USIKU, KWA SIKU ZA JUMATATU HADI JUMAMOSI . VITUO VYA TRENI YA JIJI NI DAR STESHENI, KAMATA, BUGURUNI, BUGURUNI KWA MNYAMANI, TABATA MATUMBI, TABATA MWANANCHI, MABIBO NA UBUNGO MAZIWA!
TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI KUBORESHA HUDUMA HII.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano
kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo A.Kisamfu
Dar es Salaam.
Oktoba 27, 2012


This is a brilliant idea! If it is to succeed the following should be adhered to: 1. Payment of fares - nchi hii watu wengi irresponsible, ihakikishwe nauli inalipwa na ticket inatolewa 2. Timetable iwe reliable 3. Use ICTs, kwa mfano, smart cards as tickets, payment by Mpesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Zantel Ezy pesa 3. Pawepo na business plan ya kujenga routes zingine 4. Management ya TRL isimamie hili professionally 5. SUMATRA isimamie hili, na waexamine possibilities za kuinvolve private sector. I have more ideas, lakini kwa hivi sasa nawasilisha.
ReplyDeleteDuh hii safi sana...Hongera sana wote mliofanikisha mradi huu.Haya ndiyo mambo tunayotaka kusikia serikali ikifanya.Tumechelewa lakini siyo sana.
ReplyDeleteWazo la mkuu hapo juu kuhusu ununuaji wa tiketi kwa kutumia teknolojia ya kisasa lizingatiwe,litasaidia.Abiria awe na uwezo hata wa kununua tiketi za mwezi mzima kupunguza usufumbufu.
David V
Kampuni ya Selcom ndio itayoanza kuuza tiketi kwa kutumia IT softwear! Mamlaka ya kuendesha itaundwa pamoja na kushirikisha sekta binafsi! TRL kwa sasa itaatamia huduma hii hadi mchakato wa kuunda Dar Commuter Authority utakapokamilika! Endeleeni kutoa ushauri sasa na wakati itakapokuwa huduma inaendelea kutolewa tunauhitaji ili tuwahudumie vizuri zaidi!
ReplyDeleteThis is very brilliant. Ninawapongeza wote mliofanikisha zoezi hili. Mungu awababariki.
ReplyDeleteNinaomba tu iwepo transparency katika mapato na matumizi ya safari za treni. Kuwepo pia na uhakika kuwa pesa inayoingia inaweza kulipia gharama za matengenezo (maintenance) ya treni na pia kurudisha gharama za uendeshaji (running cost) ... ile inayobaki ipigiwe mahesabu ya kununua (replacement) ya mabehewa au treni mpya siku za usoni.
Asante.