Mmoja wa Maofisa wa Polisi akielekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga (tatu shoto) ,ACP Kilonzo kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi (mwenye miwani) pamoja na ASP Msuyale ( wa tatu mstari wa nyuma) wote kutoka nchini Tanzania,kuhusiana na mambo ya usalama barabarani.

Moafisa hao wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania walikuwa nchini Ujerumani kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja (21/10 - 27/10/20120),katika jimbo la Lower Saxon,ambapo pia walitembelea Mji mkuu wa jimbo hilo Hannover, Neunberg, na Gottingen. 

Aidha ziara hiyo ilihusisha mambo mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha, na rader ya kawaida, ukaguzi wa malori ya mizigo na mambo mengine mengi..
Mmoja wa Maofisa wa Polisi (mwenyeji) akiwaelekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo  pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) namna ya matumizi  mbalimbali ya usalama barabarani.
Mmoja wa Maofisa wa Polisi akimuelekeza Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga namna ya kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha kuhusiana na uendeshaji magari barabarani.
Maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania,Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo  pamoja na ASP Msuyale wakielekezwa namna ya leseni za madereva zinavyokuwa. 
Maofisa wa juu wa kutoka jeshi la polisi nchini Tanzania, Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo  pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao.Picha zote kwa hisani ya SACP Mohammed Mpinga - CO Traffic.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. mukiwaachia mda mrefu hayo makoti ya PILIZEI ...wataombea rushwa gapo hapo ujerumani hao watakuwa mapolisi weusi hao.... musicheze na mapolisi wetu

    ReplyDelete
  2. Wenzenu huku hawaombi rushwa. Mtu akifanya kosa anaandikiwa faini yake analipa bila maneno! Sasa hapo nyi mmejifunza nini? Mana tunajua wakuu wote wana mafungu yao kila mwezi toka kwa askari wadogo! Usipofanya hivyo ujue utatolewa na kuwa FFU kusubiri fujo. Tuelezeni mmefaidika na nini muwafundishe madereva wa hapa nyumbani?

    ReplyDelete
  3. Wameenda huko wajifunze kweli na waje wayafanyie kazi waliyojifunza huko wakirudi nyumbani.Siyo kwenda kutembea tu halafu wakirudi nyumbani wanaendeleza madudu wanayofanya kila siku.

    ReplyDelete
  4. Jamaa Anonymous wa Tue Oct 30, 06:49:00 PM 2012;
    Umeniacha hoi, mbavu sina.

    ReplyDelete
  5. Hata wapelekwe Ulaya rushwa hawataacha, kupoteza muda bure tu wa kuwapeleka Ulaya

    ReplyDelete
  6. Tehe tehe teheee...kweli anomymous wakwanza hapo juu hufai hata kidogo...tihi tihi tihiiii....nahisi hapo watakua wanayatamani sana hayo magari yanayopita but sijui kama kijerumani kinapanda au walikua wanawasiliana kwa ISHARA maana wajerumani wengi hawapendi kiingereza na hutukuza zaidi lugha yao.

    ReplyDelete
  7. Mie naishi ujerumani kwa miaaka mungu haimaanishi chochote kuomyeshwa hivyo wasijitie maofi wala Nini haimaanishi chochote washamba wakubwa kudanganya watu .

    ReplyDelete
  8. Ughaibuni rushwa pia ipo. Kuna rushwa ya ngono, ambayo ni mbaya zaidi ya rushwa ya pesa.

    ReplyDelete
  9. Haya copy huko mje ku-paste huku kama mlivyo-copy na kupaste leseni za udereva za south africa bila kujali mazingira na katiba ya nchi inasemaje muanzishe zogo jingine mpate nafasi ya kupiga virungu wananchi kama si kuwa-mwangosi.

    ReplyDelete
  10. Halafu hawana hata vi-note book naona wameweka mikono mifukoni, wataweza kukumbuka kila kitu? Wabongo bwana!

    ReplyDelete
  11. Unamchukua jangili kwenda kujifunza jinsi ya kuhifadhi wanyama!

    ReplyDelete
  12. DAH HAPO NILICHOKIONA KWA HARAKA NI TOFAUTI YA KIMO, HEBU ANGALIENI HEIGHT YA HAO ASKARI WA KIJERUMANI HALAFU TAZAMENI NA WAKWETU, KUMBUKA HAO WA KWETU WALICHAGULIWA KWA KIGEZO CHA UREFU PIA, YAANI HAO NDIO WAREFU WETU... DAH MAMBO YA BINAADAM HAYO

    ReplyDelete

  13. Inaelekea hawakupata muda wa kuangalia jinsi ya kung'ang'ania madaladala na magari ya mkaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...