Mmoja wa Maofisa wa Polisi akielekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga (tatu shoto) ,ACP Kilonzo kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi (mwenye miwani) pamoja na ASP Msuyale ( wa tatu mstari wa nyuma) wote kutoka nchini Tanzania,kuhusiana na mambo ya usalama barabarani.
Moafisa hao wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania walikuwa nchini Ujerumani kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja (21/10 - 27/10/20120),katika jimbo la Lower Saxon,ambapo pia walitembelea Mji mkuu wa jimbo hilo Hannover, Neunberg, na Gottingen.
Aidha ziara hiyo ilihusisha mambo mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha, na rader ya kawaida, ukaguzi wa malori ya mizigo na mambo mengine mengi..
Mmoja wa Maofisa wa Polisi (mwenyeji) akiwaelekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) namna ya matumizi mbalimbali ya usalama barabarani.
Mmoja wa Maofisa wa Polisi akimuelekeza Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga namna ya kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha kuhusiana na uendeshaji magari barabarani.
Maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania,Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale wakielekezwa namna ya leseni za madereva zinavyokuwa.
Maofisa wa juu wa kutoka jeshi la polisi nchini Tanzania, Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao.Picha zote kwa hisani ya SACP Mohammed Mpinga - CO Traffic.
mukiwaachia mda mrefu hayo makoti ya PILIZEI ...wataombea rushwa gapo hapo ujerumani hao watakuwa mapolisi weusi hao.... musicheze na mapolisi wetu
ReplyDeleteWenzenu huku hawaombi rushwa. Mtu akifanya kosa anaandikiwa faini yake analipa bila maneno! Sasa hapo nyi mmejifunza nini? Mana tunajua wakuu wote wana mafungu yao kila mwezi toka kwa askari wadogo! Usipofanya hivyo ujue utatolewa na kuwa FFU kusubiri fujo. Tuelezeni mmefaidika na nini muwafundishe madereva wa hapa nyumbani?
ReplyDeleteWameenda huko wajifunze kweli na waje wayafanyie kazi waliyojifunza huko wakirudi nyumbani.Siyo kwenda kutembea tu halafu wakirudi nyumbani wanaendeleza madudu wanayofanya kila siku.
ReplyDeleteJamaa Anonymous wa Tue Oct 30, 06:49:00 PM 2012;
ReplyDeleteUmeniacha hoi, mbavu sina.
Hata wapelekwe Ulaya rushwa hawataacha, kupoteza muda bure tu wa kuwapeleka Ulaya
ReplyDeleteTehe tehe teheee...kweli anomymous wakwanza hapo juu hufai hata kidogo...tihi tihi tihiiii....nahisi hapo watakua wanayatamani sana hayo magari yanayopita but sijui kama kijerumani kinapanda au walikua wanawasiliana kwa ISHARA maana wajerumani wengi hawapendi kiingereza na hutukuza zaidi lugha yao.
ReplyDeleteMie naishi ujerumani kwa miaaka mungu haimaanishi chochote kuomyeshwa hivyo wasijitie maofi wala Nini haimaanishi chochote washamba wakubwa kudanganya watu .
ReplyDeleteUghaibuni rushwa pia ipo. Kuna rushwa ya ngono, ambayo ni mbaya zaidi ya rushwa ya pesa.
ReplyDeleteHaya copy huko mje ku-paste huku kama mlivyo-copy na kupaste leseni za udereva za south africa bila kujali mazingira na katiba ya nchi inasemaje muanzishe zogo jingine mpate nafasi ya kupiga virungu wananchi kama si kuwa-mwangosi.
ReplyDeleteHalafu hawana hata vi-note book naona wameweka mikono mifukoni, wataweza kukumbuka kila kitu? Wabongo bwana!
ReplyDeleteUnamchukua jangili kwenda kujifunza jinsi ya kuhifadhi wanyama!
ReplyDeleteDAH HAPO NILICHOKIONA KWA HARAKA NI TOFAUTI YA KIMO, HEBU ANGALIENI HEIGHT YA HAO ASKARI WA KIJERUMANI HALAFU TAZAMENI NA WAKWETU, KUMBUKA HAO WA KWETU WALICHAGULIWA KWA KIGEZO CHA UREFU PIA, YAANI HAO NDIO WAREFU WETU... DAH MAMBO YA BINAADAM HAYO
ReplyDelete
ReplyDeleteInaelekea hawakupata muda wa kuangalia jinsi ya kung'ang'ania madaladala na magari ya mkaa.