Leo mchana nimepita katika eneo hili la kijiji cha karibu na Hedaru,Mkoani Kilimanjaro nikiwa katika safari yangu ya kuelekea jijini arusha na nimepatwa na mshangao mkubwa sana pale nilipoona katika barabara kubwa kama hii imewekwa mawe makubwa makubwa (yanaonekana pichani) sijui hata ni kwaajili ya nini.nilishangazwa sana na tukio hilo kwani killa nilipojaribu kuangalia kushoto na kulio kuona kama nitamuona mtu hata mmoja ili nimuulize juu ya hili,hata sikufanikiwa.maana mawe haya yamewekwa bila tararibu yeyote ya kiusalama barabarani kufuatwa,yaani kwa maana hiyo yamewekwa kienyeji.

Ankal naomba uitupie hii ili wadau waweze kuona na kutoa maoni yao maana hali hii ni ya hatari sana,kwani inaweza sababisha hata ajali na watu wakapoteza maisha.

Mdau wa Globu ya Jamii
Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hukuchukua muda wa kututafuta, mbona tulikuona unakuja kwa mbali tulihisi ni msafara wa rais na ndiyo maana tulijificha. Tuna machungu sana na hii nchi, vijana wengi hatuna kazi na ndiyo maana tunatoa hasira zetu kwa Fiesta tukifanya ujinga na ufuska bila kupingwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani raisi ndio atakufanya uwajibike? Mashamba yamejaa kibao, mnashindwa kulima mnatafuta tuu mtu wa kumpa lawama, ulitaka raisi akupe hela? Ninyi ndio mnaipotosha maadilifu, naomba Mungu uwe huna watoto maana wataiga mfano gani kama wewe ndio mawazo yako yashakinga ukuta wa kupewa bila jasho?!!!

      Delete
  2. kwanini usijitolee kuyatoa? au ndio unangojea serikali iyatoe?Hebu jamani tuache mambo ya uvivu na kulalamika.

    ReplyDelete
  3. Hao ni askari wa usalama barabarani waliweka kizuizi ili watu wasikatae kusimama...thatha wewe unadhani wao watakula wapi avae? Ni afadhali ugumirije du avae...nilo isanga letu ilo..swi tutonge tuela miguva uko ugu Kithiwani...na chome...!! Mdau-USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...