Mgambo wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, "wakihangaika" na mikokoteni iliyobeba matunda, wakijiandaa kuvuka barabara ya Nyerere eneo la Kamata kuelekea ghala la Manispaa hiyo. Mashuhuda walisema, mikokoteni hiyo waliikamata kutoka kwa wachuuzi wadogowadogo maarufu kama Wamachinga, wakidai kuwa hawana ruhusa ya kufanya biashara holela.Picha na K-Vis Blog
Home
Unlabelled
Mgambo wa Jiji la Dar wakiwa kazini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hao wachuuzi wakale polisi? ndio maana mageuzi yanahitajika huu ni unyanyasaji wa wananchi. sehemu zilizotengwa wanapewa watu wenye nazo maana hawa hawanauwezo hata wa kujenga vibanda vya biashara uonevu mkubwa sana huu. Mungu atawaona.
ReplyDeletewow mbona rahisi kuwa shika wamachinga wanao tafuta chakula kwa hali ngumu na ya haki lakini mafisadi mbona hamuwashiki hivyo ...nyie mgambo ndiyo maana hamlipwi miezi maana mnawasikiliza wanaowatesa.
ReplyDeletejiungeni na vyama vya upinzani ili nanyi muache kuwaonea wenzenu eti kwa vile mnamagwanda
Vijana wanajitafutia kipato lakini mnawanyanyasa, kwanini pasiwe na njia ya hao vijana kupata vibali kufanya hiyo biashara. Wakikosa kwa njia hii jueni kuwa itabidi njia mbadala ipatikane, msibaki kulialia tu wakichaijua hiyo njia nyingine"!!
ReplyDeleteHUU NI UONEVU NA UNYANYASAJI WA HALI YA JUU. VIJANA WAMEJITENGENEZEA KIFAA CHA KUTEMBEZA DUKA LAO NA TAKA WANATEMBEA NAZO. KULIKONI MGAMBO WAWA NYANYASE?? WANATAKA WARUDI MITAANI KUPIGA KABARI?? TUNAKWENDA WAPI TANZANIA????
ReplyDeleteMtaji wa huyo muuza matunda 10.000! Anaiheshimu kazi yake anayoifanya kwani ndio inayomlisha na mahitaji mengine yote anapata toka hapo! Sasa we mgambo unaependa sifa kuonyesha unafanya kazi yako! Ungeanza na wala rushwa bila kijali ni nani ndio ningekuona una uchungu! We mwenyewe maskini huna mbele wala nyuma! Ukipata tatizo hapo hata huyo aliekutuma haji kukusaidia! Leo unamkamata mtu aliyekopa 10.000 ili ajisaidie kimaisha unataka huyo mtu afanye nini? Mana hayo matunda ni chakula bora na ndio yanaleta vitamini hata kwa hao mabosi wako wakiwekewa chakula hawakosi matunda! Huo ni uonevu mkubwa sana ila siku zenu sio nyingi watu wakiamua mtspata shida sana nyie waoneaji wakubwa.
ReplyDeleteHebu wangalie kwanza na wakivaa hayo magwanda wanaona sifa, hebu wawache wenzao wajitafutie riziki, michosho sana hawa mgambo si waende wakawakamate mafisadi kwanza, wanoharibu kila kitu katika hii nchi, kwa kukosa maendeleo, ya huduma muhimu kama, hospital, barabara nzuri, mazingila mazuri ya usafi, na kuvutia, mafisadi wanapendezesha mahekaru yao tu, na kwa kuibia hii nchi.
ReplyDeleteSUBHANAALLAH!! WALLAH HII SIO HAKI KABISA, HAWA WATU WAKALE WAPI JAMANI?????? MBONA MNAWANYANYASA????????
ReplyDeleteNyie watoa maoni ni kama hamna akili vile, uonevu wapi wakati jiji chafu, mngesema mgambo wafanye kaz za kusafisha jiji ningeona wa maana eti wakamate mafisadi!!!? Mgambo akamate FISADI??? Acheni upuuzi aaghh
ReplyDeleteTuwe na utamaduni wa kufuata sheria, taratibu na kanuni. Dar ni jiji ambapo popote ni soko, choo, njia, ofisi,grosary, stendi nk... hebu fikiria una nyumba yako ukute mtu kalala bafuni, anafua chumbani,anapumzika chooni, anajisaidia kibarazani! Ustaarabu gani huo.
ReplyDeleteWakiwa katika kazi ya unyang'anyi au? Wahuni wakubwa hapo wanashangilia familia zao leo zitafaidika kwa unyanyasaji wanaofanyia wengine. Ni laana tu kama kula moto. Watajibu kwa Mwenyezimungu
ReplyDeleteHawa wamachinga wanachafua mazingira na pia hawana leseni.kwani ni lazima wabaki Dar kwanini wasiende mikoani wakashiriki kilimo kwanza?
ReplyDeleteHAAH! ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA..MMH! WAPI Mkuu wa Mkoa DSM, Wakuu wa Wilaya zote 3, mameya wanafanya nini? Mpaka leo hii solution ya wamachinga wameshindwa kutoa, machinga complex n.k. JIJI HILI NI CHAFU NA SIO WAMACHINGA, HIZI HIZI TAKATAKA ZA MAJUMBANI AMBAZO HATUONI MAGARI YAKIPITA KUZOA, JE ZIMETOKANA NA WAMACHINGAAA!!!???.
ReplyDeleteHii ni changamoto kwenye ninyi mnaona huo niuchafu, waende wapi au mnataka wawe vibaka halafu tuanze kulalama? Vibaka wamejaa kibao hapo DARAJA LA SALENDER AMBAPO NI MITA CHACHE TU TOKA KITUO CHA POLISI, TIBA YAKE HAIJAPATIKANA TENA MNATAKA KUWASUMBUA NA HAO WACHINGA NAO WAJE WATUMALIZE?
Jiji hili ni chafu kuliko hayo matolori, njooni huku Wilaya ya Kinondoni hususani maeneo ya Mtogole, Sinza, M/nyamala/ Makumbusho/Kijitonyama, Mikocheni, manispaa imeshindwa kusafisha mitaro, kufagia barabara, hadi wakazi wa maeneo hayo naona wanasafisha mitaro hiyo na hawana pakumwaga taka wanaweka barabarani. Manispaa ya K'ndoni imeshindwa kufanya jitihada hata ya magari ya TAKA! Naona magari ya Taka yapita barabara baadhi tu kufanya window dressing. Fanyeni kazi jamani si kuzunguka kwenye viti na kusubiri warsha, semina, mambo ya serikali n.k. Acheni viti hivyo tokeni muangalie maeneo yetu ni MACHAFU SANA, BARABARA ZIMEMEZWA/KUFUNIKWA NA MCHANGA.