Mkutano mkuu wa watanzania waishio ujerumani uliofanyika siku ya Jumamosi  tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake Moja wapo ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo, kabla ya kufanyika uchaguzi huo na mjadala wa maazimio ya umoja huo.

Mgeni rasmi katika mkutano huo mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa ambaye alitoa nasaha zake na salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria katika mkutano huo. Kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa kuunda umoja huo wa watanzania waishio ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote nchini ujeruman.

Isitoshe Bw. Ali Siwa aliwaambia watanzania kwamba ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri wowote utakaoleta maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla, aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa ufunguo na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani pia. baada ya nasaha hizo wananchama wa umoja wa watanzania walichagua viongozi wao kama ifuatavyo:- 

 Mwenyekiti: Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel. Umoja huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria, ambacho kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja linalowaunganisha watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni. Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani (UTU) milango ipo wazi, wasiliana na kamati.utu@googlemail.com
 Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU mara baada ya mkutano huo

 Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani
Wadau wakifurahia
Kamanda Ras Makunja wa FFU (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kutoroka lindo ili kuhudhuria mkutano huu

 Kamanda Ras makunja katikati,akipigwa pini na Sudu Mnete wa Radio DW (shoto) na  Mdau Elezius naye pembeni
 Mwanadiplomasia Naibu balozi Bw.Ali Siwa (katikati)akiongea na watanzania
 Watanzania Ujerumani wakiduarika.
Naibu Balozi Mhe Bw.Ali Siwa akiduarika na waTanzania Ujerumani huku Kamanda Ras Makunja akimpa taffu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nimefarijika saana kwa mara ya kwanza nikimshuhudia Kamanda wa Mapambano, wa Kikosi cha Mapambano Ughaibuni RAS-MAKUNJAS akiwa amevua magwanda ya Kijeshi yenye Medali lukuki mabegani na katika Kikao cha UTU akijinafasi ndani ya SUTI NA KOTI !

    Isipokuwa 'TAHADHARI' ukimwona Simba anasinzia usichezee sharubu zake!,,,unaweza kufariki ghafla,,,unafikiri akizinduka utapona?

    ReplyDelete
  2. Kamandaz Ras Makunjaz ndani ya suti, koti na tai!

    Si mchezo Mkubwa wa Kikosi cha FFU Ughaibuni umeng'ara haswaaaa!

    ReplyDelete
  3. Ukimwona Afande Ras Makunjas Mkuu wa FFU akiwa amevaa koti, suti na tai huku hana silaha mgongoni ama begani, hata siku moja usifikiri yupo Likizo !

    Anaweza kuwa yupo zamu ktk jukumu 'maalum' amepangiwa.

    Jaribu uone utashuhudia anapapasa mfuko wa koti lake na kutoa Bastola!

    ReplyDelete
  4. Kamanda wa kikosi kazi FFU Ras Makunja ametoka chicha ! lakini siwezi kuamini kuwa yupo likizo najua ikitokea fujo tu hapo lazima virungu vitembezwe

    ReplyDelete
  5. Kikamanda ketu nacho kilikuapo? kamanda umepigwa pini? lakini nakuaminia zikitokea fujo tu unajua wajibu wako

    ReplyDelete
  6. kamanda wa ffu ras makunja kwanini umetoroka lindoni? harafu umevua magwanda na kutinga na suti kwa ati!
    hii kitu sikuingine usifanye kuliacha lindo bila ya kamanda

    ReplyDelete
  7. eh! bwana he! Kamanda ndani ya nyumba tena kwa suti kali,siyo bure lazima kulikua na neno,cha ajabu bunduki na miwani kasahau!

    ReplyDelete
  8. kamanda ras makunja bila magwanda,huo mkutano kweli uliaminika ,naona siku hiyo majukwaa yalipumzika? sasa kamanda mie nimefika bei suti? na viatu nataka nikuvue nipe bei?

    ReplyDelete
  9. kamanda mkuu wa ffu ras makunja kwa nini?umetoroka lindoni,lakini umependeza,hiyo ndio suti ulinunuliwa na baba wa kambo? harafu utaenda kumuimba jinsi ulivyokosa adabu

    ReplyDelete
  10. kamanda lazima tufukuze kazi kwa kosa la kutoroka lindoni na kukimbilia mduara

    ReplyDelete
  11. hongereni sana watanzania wa ujerumani nyinyi hamna matawi ya vyama vya kisiasa bali mnashikamana nawaombeni mbaki na mfumo wenu huo huo

    ReplyDelete
  12. Mkuu kamanda wa ffu ras makunja,mie nina swali nauliza mbona ubavuni kwako koti limetuna? au kuna chamoto?

    ReplyDelete
  13. Mkuu kamanda wa ffu ras makunja,mie nina swali nauliza mbona ubavuni kwako koti limetuna? au kuna chamoto?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...