JUMUIA ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ipo katika mpango maalum wa uboreshaji wa Maktaba ya Picha za kumbukumbu ya Matukio ya Kihistoria na vitu mbalimbali vinavyohusiana na Umoja huo kwa nchi zote wanachama.

Kazi ya Upigaji picha hizop inafanywa na Wapiga picha bora kumi kutoka jumuia hiyo ambao mara baada ya kupatikana walipatiwa Mafunzo maalum ya upigaji Picha na Utengamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki mjini Arusha chini ya Shirika la Kijerumani la GIZ.

Zoezi la upigaji picha hizo zilizo katika ubora wa hali ya juu ulianza juma lililopita Nchini Kenya na sasa timu ya Wapigapicha hao wapo Nchini Tanzania na wameanzia katika Kisiwa cha Zanzibar ambacho kipekee katika mambo muhimu ya EAC kina mambo mebngi ya Kihistoria.

Pichani ni Kundi la Wapiga picha hao Mroki Mroki (katikati), Filbert Rweyemamu (kushoto) wakiongozwa na Mtaalam Harmut Fiebig (wapili kulia) kutoka nchini Ujerumani ambaye anafanyia Shughuli zake nchini Kenya. Wengine katika picha hiyo ni Mpigapicha wa Kujitegemea Zanzibar Martin Kabemba kulia na Ofisa Kutoka Kitengo cha Habari EAC, Suk Chat.
 Bendera ya EAC ikipepea katika Jahazi Kisiwani Zanzibar
 Wakionesha Mtangamano kwa kugonganisha vikombe vyao vya Kahawa
 Misikiti ya kale

 Majengo ya Kale ya Kihistoria ni moja ya picha zitakazo hifadhiwa katika Maktaba hiyo ya Picha ya Jumuia ya Afrika Mashariki, na Endapo Wanahabari, na watafiti watahitaji kuzitumia basi zitapatikana kwa urahisi.

 Mahabusi ya Watumwa Zanzibar
Sanamu za Watumwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Picha ya tatu kutoka juu:

    Cheers ya Vikombe vya kahawa nimeipenda!

    Ugonganishaji wa vikombe vya kahawa nimeupenda!

    ReplyDelete
  2. Pia wakusanye picha za kihistoria za zamani katika maktaba mbalimbali na kwa watu binafsi walizozikusanya kama ukumbisho.

    ReplyDelete
  3. wazanzibari na wanauamsho watakuja juu jamani na hizo picha zenu. wanadai zanzibar kulikuwa hakuna utumwa mnawasingizia tu.

    ReplyDelete
  4. kwa nini wanonyesha kila mara utumwa kwani huko bara utumwa ulikuwa haupo wazungu utumbwa wao ndo mbaya kuliko wote

    ReplyDelete
  5. nilijua hutoweka comment yangu nimeingai hapa kuangalia kama umeiwekau unahaki ya kuweka au kutokuweka mkuuu ndo blog yako lakin nakuambia hivi na wewe pia fisadi unakula sahani mmojana mafisadi wa nchi hii

    mdau u.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...