Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Alli Mcharazo akitoa taarifa yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Maktaba kwa maendeleo leo jijini Dar es Salaam ambao umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Selestine Gisimba (hayupo pichani).
Mratibu wa Mradi wa chama cha wakutubi kutoka Finland (TLF) Marjatta Lahthi akitoa taarifa yake katika ufunguzi wa mkutano wa maktaba kwa maendeleo jijini Dr es Salaam leo ambapo umewashirikisha zaidi ya watu 80 wakiwemo wadau wa maktaba pamoja na wajasiriamali kutoka Tanzania, Kenya,Finland,Gemany, Italy na United Kingdom. Mradi huo kupitia maktaba pamoja na mtumizi ya teknolojia ya ICT utawawezesha kupata habari mbalimbali za shughuli zao za kila siku.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Libraries for Development wakiwa katika mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Selestine Gisimba (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha washiriki wapatao 80 kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, Finland, Germany, Italy na United Kingdom. Mradi huo wa Maktaba kupitia teknolojia ya ICT utawawezesha kuwasaidia kupata elimu na taarifa mbalimbali za shughuli zao za kila siku.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Selestine Gisimba (wa pili kulia alievaa suti) , Mwenyekiti wa Bodi ya TLSB Prof. Mathew Luhanga (kulia) pamoja na washiriki wengine wa mkutano wa Maktaba kwa maendeleo wakifuatllia mkutano huo kwa makini leo jijini Dar es Salaam, Mkutano huo umewashirikisha washiriki wapatao 80, kutoka nchi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, Baada ya kupata elimu na uzoefu kupitia teknolojia ya ICT, wadau hao watapata taarifa mbalimbali kwaajili ya matumizi ya shughuli zao za kila siku.
Mwenyekiti wa Bodi ya TLSB nchini Prof. Mathew Luhanga (kushoto) akibadilishana mawazo baada ya ufunguzi wa mkutano wa maktaba kwa maendeleo Okt. 16,2012 jijini Dar es salaam(katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa Maktaba ya Taifa Dkt. Alli Mcharazo na (kulia) na Mratibu wa mradi wa chama cha Wakutubi kutoka Finland (FLA) Majatta Lahthi.


+pamoja+na+Mwenyekiti+wa+Bodi+ya+TLSBProf.+Mathew+Luhanga+(kulia)+wakifuatilia.jpg)
+akibadilishana+mawazo+na+Mkurugenzi+Mkuu+wa+TLSB+Alli+Mcharazo+(katikati.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...