Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magessa Mulugo akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarim Jonjo anayeuguza majeraha aliyoyapata baada ya kutupiwa bomu nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo eneo la mtaa wa kanisani kata ya Sokoni jijini Arusha.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Afande Liberatus Sabas akiangalia maganda yanayosadikiwa kuwa ya hilo bomu lililotipiwa dirishani katika nyumba ya Katibu wa BAKWATA wa mkoa huo usiku wa kuamkia leo
Dirisha lilikotupiwa hilo bomu.
Picha zote na Mahmoud Ahmad

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sasa hawa askari wanaposhika hayo maganda ya mabomu bila hata kuvaa glovu hawawezi kuharibu ushahidi wa kuwapata watuhumiwa kweli? Mimi sio askari wala mpelelezi lakini naelewa njia mojawapo ya ushahidi wa kuwapata watuhumiwa (wahusika) ni kuchukua alama za vidole kwenye hayo maganda na kuyafananisha na alama za vidole za watuhumiwa. Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. Mbona Kova mwenyewe anashika kwa mikono mikavu bunduki za wahalifu?

    ReplyDelete
  3. tanzania bado hatujaendelea katika nyanja hizi so msiwalaumu hawa maaaskari wadau wenzangu sisi tuliopo majuu ndo tunaona dosari hizi lakini kwao ni jambo la kawaida kwenda mbele.

    ReplyDelete
  4. sasa kama huyo askari ndiye aliyetupa hilo bomu si tushapoteza ushahidi

    ReplyDelete
  5. naam tumeshapoteza ushahidi na naumunga mdau hapo jua aliyeseama bado hatujafika huko tukiwa majuu ndo tunajua athari hiizi lakin bongo ndo bongo tena kibongo bongo ili mradi riski ipite kooni.

    na pia inawezekana hao hao maaskari wameweka hayoa mapombu binadamu wabaya wee usisikiye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...