Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magessa Mulugo akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarim Jonjo anayeuguza majeraha aliyoyapata baada ya kutupiwa bomu nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo eneo la mtaa wa kanisani kata ya Sokoni jijini Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Afande Liberatus Sabas akiangalia maganda yanayosadikiwa kuwa ya hilo bomu lililotipiwa dirishani katika nyumba ya Katibu wa BAKWATA wa mkoa huo usiku wa kuamkia leo
Dirisha lilikotupiwa hilo bomu.
Picha zote na Mahmoud Ahmad


Sasa hawa askari wanaposhika hayo maganda ya mabomu bila hata kuvaa glovu hawawezi kuharibu ushahidi wa kuwapata watuhumiwa kweli? Mimi sio askari wala mpelelezi lakini naelewa njia mojawapo ya ushahidi wa kuwapata watuhumiwa (wahusika) ni kuchukua alama za vidole kwenye hayo maganda na kuyafananisha na alama za vidole za watuhumiwa. Nawasilisha
ReplyDeleteMbona Kova mwenyewe anashika kwa mikono mikavu bunduki za wahalifu?
ReplyDeletetanzania bado hatujaendelea katika nyanja hizi so msiwalaumu hawa maaaskari wadau wenzangu sisi tuliopo majuu ndo tunaona dosari hizi lakini kwao ni jambo la kawaida kwenda mbele.
ReplyDeletesasa kama huyo askari ndiye aliyetupa hilo bomu si tushapoteza ushahidi
ReplyDeletenaam tumeshapoteza ushahidi na naumunga mdau hapo jua aliyeseama bado hatujafika huko tukiwa majuu ndo tunajua athari hiizi lakin bongo ndo bongo tena kibongo bongo ili mradi riski ipite kooni.
ReplyDeletena pia inawezekana hao hao maaskari wameweka hayoa mapombu binadamu wabaya wee usisikiye