MWANAJESHI mmoja amekufa na mwingine kujeruhiwa baada ndege ya mafunzo waliyokuwa wakiendesha kushindwa kupaa kwa kujipiga bawa kwenye hanga Uwanja wa Ndege wa Jeshi, Airwing, Ukonga, Dar es Salaam leo. 

Akielezea juu ya ajali hiyo, Msemaji wa Jeshi la ,Kanali Kapambala Mgawe, alitaja jina la aliyepoteza maisha kuwa ni Kapteni Mangushi na aliyejeruhiwa kuwa ni Kampeni Kilikila. 

Alisema kuwa wanajeshi hao wote walikuwa ni wanafunzi na walikuwa kwenye mafunzo ya kawaida, ambapo waliipanda ndege hiyo ya kivita huku wakiwa na miavuli, na baada ya kuruhusiwa walifyatua kitufe cha kupaa ndege, lakini bahati mbaya ilishindwa kwenda angani na paa lake kugonga hanga la kutengenezea ndege. 

Ndege hiyo ilitakiwa iruke kwa spidi kubwa mithili ya risasi umbali wa mita 100 kwenda angani. Aliendelea kusema kuwa ndipo wanajeshi hao waliokuwa wamevaa miamvuli walitupwa nje, ambapo mmoja aliyejeruhiwa baada ya kuangukia kwenye lami barabarani na aliyekufa alijigonga juu ya paa la hanga baada ya mwavuli aliokuwa nao kushindwa kufunguka. 

 Mgawe anasema kuwa kawaida tahadhari zinakuwepo, ila kwa tukio hilo bado hawajatambua tatizo lilikuwa ni nini. Anasikitika kumpoteza mmoja wa wanajeshi wapiganaji hao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Napenda kutoa pole kwa wananchi, jeshi na familia kwa kupoteza ndugu yetu vilevile mungu ampe nafuu na afya njema majeruhi.Ni jambo la kawaida sana kutokea ktk mafunzo haya nakumbuka nilipokua ukraine 2011 ndege ya mafunzo yenye wanafunzi 4 ilizimika ikiwa angani na miavuli waliyokuanayo hao wanafunzi baadhi haikufunguka hivyo walipona wawili na wengine walikufa.

    ReplyDelete
  2. michuzi bawa la ndege liligonga hanga, halafu tena paa la ndege liligonga hanga? hanga ni gereji ya ndege, ndege hazianzi kuruka katika hanga, bali safari ya kwenda kuruka inaweza anzia hapo.
    ngoja nikurekebishie taarifa hii kidogo, walipoingia kwenye ndege tayari kwenda kuruka wakabonyeza kitufe cha kuwatoa kwenye ndege inapokuwa angani wakati wa dharura, lakini wao walikibonyeza ndege ikiwa chini karibu na hanga, kwa hiyo walirushwa nje, mmoja akajigonga chini ya paa la hanga na wapili alirushwa juu na kurudi chini bila miavuli yao kufunguka sawasawa ili kuwaokoa na madhara makubwa, kwani kima walichorushwa hakikuwa cha kutosha miavuli kufunguka inavyostahili.
    anyway tujipe pole msiba wetu wote.

    ReplyDelete
  3. I LIKE AFRICANS......kwa sababu ilitokea ukraine na watu walikufa ni jambo la kawaida, kweli akili zetu sisi waafrica bado hazijakuwa hata kidogo, watakakunambia kwa vile ajali za gari zinatokea marekani au ulaya ni jambo la kawaida na hapa kwetu watu wafe, wewe ni mtu wa aina gani mwenye mawazo finyu namna hii na pengine uko sehemu nyeti kabisa au ndio nyinyi munaopanda jukwaani mukasema tanzania ni muungano wa PEMBA NA ZIMBABWE

    wacha watu wafanye uchunguzi wa ajali na kwanini itokee hivyo mpaka askari wetu kufariki kwenda kwako ukraine isiwe sababu ya vifo hapa kwetu au wewe ndie kipofu ulieona jogoo kwa siku ya kwanza kuona,

    ulaya kitokeapo kitu hicho wanapitisha uchunguzi wa kina kujuwa tatizo sio ni kawaida tu kwa vile ati ukraine walikufa mtu kama wewe hufai hata kutoa maoni kumbuka kuwa hapa kafa mtu halafu unasema ni kitu cha kawaida,

    na kupeleka jeshi mukapiga watu kariakoo vile vile ni jambo la kawaida au hili hukuliona kule ukraine ulikokwenda,

    sasa swali munaulizwa kama kariakoo mulipeleka jeshi kuzuia watu je malawi mutapeleka nini

    ReplyDelete
  4. Kila gazeti linasema kivyake, tumwamini nani? Hebu soma magazeti kama nane hivi ya leo ujionee maajabu ya makanjanja na waandishi.Msiahangae watoto kumaliza shule bila kujua kosoma na kuandika vishangaeni vyombo vya habari na wahariri wao.

    ReplyDelete
  5. What in heaven is going on with the preceding commentators ? Must be comments submitted by Robots lol

    ReplyDelete
  6. gazeti la mwananchi ndio wameharibu kabisaa! wameandika ndege imeanguka. hakuna ndege iliyoanguka uwanja wa ndege wa julius nyerere dar siku ya tukio hilo.
    waandishi fanyeni utafiti msichukue habari na kukimbilia kuandika bila kuuliza/kujiuliza maswali hata kidogo. mwananchi wamedanganya kama hawajadanganya wamesaidia kudanganya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...