Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza na maafisa wengine.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo amesema Rais amemteua Bwana John Casmir Minja (pichani) kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:
·        Dkt. Juma Ally Malewa ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na Uendelezaji wa Magereza.
 ·        Bwana Deonice Lwamahe Chamulesile ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji.
 ·        Bwana Gaston Sanga ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.
Wengine ni:
·         Bwana Fidelis M. Mboya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza na;
 ·        Bwana James B. Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine.
 Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 1, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tangu tarehe 25 Septemba, 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Afande Minja, u deserve it and much more.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...