WAREMBO 30 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanatarajiwa kuingia kambini leo kwenye hoteli ya Giraffe kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kushiriki shindano la urembo la Taifa 'Redd's Miss Tanzania 2012' litakalofanyika Novemba 3 kwenye ukumbi wa hoteli ya Ubungo Plaza hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency International, Hashim Lundenga alisema kuwa warembo wote walishapewa taarifa za kuripoti kambini leo na mara baada ya kuwasili watapewa taratibu za kambi hiyo.
Lundenga aliwataka washiriki hao kuhakikisha wanawasili asubuhi mapema katika ofisi za Kamati ya Miss Tanzania kama walivyoambiwa ili wapelekwe pamoja katika hoteli hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kambi yao ya mwezi mzima.
Alisema warembo wakiwa katika kambi ya Redd's Miss Tanzania watafundishwa mambo mengine muhimu katika maisha yao ambayo yatawafanya wajiandae kuwa wanawake walio na maendeleo na watakaokuwa tayari kuongoza familia zao.
Alisema pia baada ya kumpata mshindi atakapewa mapumziko ya miezi miwili na baadaye ataanza maandalizi ya kujiandaa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya mwakani.
Alisema kuwa licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali katika mashindano hayo, anawapongeza mawakala kwa kazi ya kusaka warembo ambao wengi wao waliofanikiwa kufuzu fainali hizo ni wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...